29.7 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kibanda: Kishindo cha Lowassa kisingekoma

*Azungumzia ndoto ya Lowassa kuandika Kitabu

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Mwenyekiti Mstaafu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF), Absalom Kibanda amesema iwapo Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa angeendelea kuwa hai kishindo chake katika Siasa za Tanzania kisingekuwa na mwisho.

Kibanda amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Meta (zamani Facebook) ikiwa ni siku chache zimepita tangu kifo cha Lowassa aliyefariki Dunia Februari 10, mwaka huu akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) jijini Dar es Salaam.

Absalom Kibanda akiwa na Hayati Edward Lowassa(kushoto).

Kibanda amebainisha kuwa Lowassa alikuwa ni mtu mkweli na mwalimu ambaye alifundisha na kuasa huku pia akiwa tayari kushaurika na kukosolewa.

“Fare thee well Edward Ngoyai Lowassa. Mtu mkweli, kweli kweli. Kwako kusamehe saba mara sabini lilikuwa ni jambo la kawaida. Ulitufundisha, ulituasa, ulikuwa msikivu sana, mcha Mungu, na rafiki wa kweli uliyekuwa tayari kushaurika na kukosolewa.

“Ulikuwa mwalimu mwema na mwanafunzi hodari. Simba angurumaye nyikani. Joto lako katika siasa za Tanzania lilitikisa hii nchi kwa miongo mitatu pasipo kukoma. Laiti kama si afya, kishindo chako kisingekoma,” ameandika Kibanda na kuongeza kuwa:

“Nimeyatunza yote tuliyoteta. Kazi uliyonipa panapo majaliwa itafanyika,” ameeleza Kibanda.

Katika hatua nyingine, Kibanda amebainisha kuwa Hayati Lowassa alikuwa mbioni kuandika kitabu cha maiha yake na kwamba tayario yeye(Kibanda) alikuwa tayari ameanza kutayarisha maudhui kwa ajili ya kuandika kitabu cha Kiongozi huyo aliyetikisa Tanzania katika nyanja ya Siasa.

“Lowassa tangu hata kabla hajagombea urais alikuwa na ndoto ya kuandika Kitabu cha Maisha yake, mimi ni miongoni mwa watu ambao Lowassa alitufuata na kunikutanisha na familia yake wakiwamo ndugu zake kwa ntakati tofauti kuhusu dhamira yake ya kuandika kitabu hicho na tayari nilikuwa nimeshafanya mahojiano na ndugu zake, dada zake, wadogo zake na nilikuwa katika maandalizi ya kufanya mkutano na yeye mwenyewe japo isivyo bahati akawa ameanza kuugua.

“Japo tayari mara kadhaa tulikuwa tumekaa naye na kuzungumza mambo mbalimbali ambayo angependa yawepo katika kitabu ambacho angekiandika yeye mwenyewe, kwa hiyo Lowassa amefariki dunia kabla ya kile alichokuwa anatamani kukifanya sana kikiwa hakijatimia.

“Yuko kijana wake ukimuacha Fredrick Lowassa(kijana wake) Hussein Mohammed Bashe(Mbunge wa Nzega Mjini ambaye pia ni Waziri wa Kilimo) ni moja ya vijana ambao tangu Lowassa akiwa na mpango wa kugombe urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) walikuwa wameshazungumza kuhusu haja ya kuandika kitabu na wote walikuwa wameniona kuwa miongoni mwa watu ambao wangeandika kitabu hicho, kwani Lowasa alikuwa mfuasi wangu mkubwa katika safu yangu ya TUENDAKO niliyoanza kuandika mwaka 2007 wakati huo Lowassa akiwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Tanzania Daima,” amesema Kibanda.

Hayati Edward Lowassa anatarajiwa kuzikwa Jumamosi Februari 17, kijijini kwao Ngarash wilayani Monduli Mkoa wa Arusha ambapo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ataongoza mazishi hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles