26.1 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yampiga mnyama pale pale

Na Winfrida Mtoi

Yanga imeendeleza ubabe mbele ya watani zao Simba baada ya leo Aprili 20,2024 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Aziz Ki dakika ya  20 kwa mkwaju wa  penalti baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya boksi na Joseph Guede dakika 38, huku bao la Simba likifungwa na  Freddy Koublan dakika 74.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kuwa mbabe kwa Wanamsimbazi hao baada ya mechi ya  mzunguko wa kwanza Novemba mwaka jana kuwafunga mabao 5-1 kwenye uwanja huo huo.

Ushindi huo unawafanya Wanajangwani hao kuendelea kukaa kileleni wakifikisha alama 58 katika michezo 22 waliyocheza, Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 46, ikicheza mechi 21.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles