26.1 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Taliss mabingwa mashindano ya Taifa ya Klabu

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Timu ya mchezo wa kuogelea ya Taliss, imeibuka mabingwa wa jumla wa mashindano ya Taifa ya Klabu baada ya kujikusanyia pointi 385.

Katika mashindano hayo ya siku mbili yaliyomalizika leo Aprili 21,2024, mshindi wa pili ni Dar Swimming iliyopata pointi 330 , namba tatu ni Mwanza Club yenye alama 96, huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Bandari ya Mombasa ikiwa na pointi 88.

Akizungumzia ushindi huo Nahodha wa timu ya Taliss, Delbert Ipilinga, amesema wamefurahi kuchukua ubingwa huo kwa mara ya sita na siri kubwa ni kujituma  katika mazoezi na kazi kubwa inayofanywa na viongozi wao akiwamo kocha.

“Nashukuru Mungu, nimeona klabu yetu tumewatendea haki meneja na kocha wetu. Tuna kocha anafanya kazi kubwa kutufanya sisi kuwa waogeleaji bora pamoja na sisi wenyewe kujituma katika mazoezi”, amesema Debert.

Ametamba kuwa wataendelea kuonesha makali yao katika mashindano mbalimbali, huku akiwataka wapinzani wao wajipange zaidi ili kuwapindua.

Naye muogeleaji wa kike wa timu hiyo, Sofia Latiff, ameeleza kuwa ushindi huo umetokana na kazi kubwa wanayoifanya kwa ushirikiano na wanatarajia kufanya vizuri zaidi.

Meneja wa Taliss, Hadija Shebe amesema  wamechukua mfululizo ubingwa huo na mwaka huu walijipanga kuhakikisha wanaendelea kushikilia taji hilo.

“Tulichowazidi wapinzani wetu ni kwenye maji pekee, kila klabu ilijipanga na timu pekee ambayo tulikuwa hatuijui vizuri ni ile iliyotoka Kenya lakini la muhimu tumefanikiwa kuwa washindi kama tulivyotaka,” amesma Hadija.

Naye kocha wa Dar Swimming ambaye pia ni  kocha wa timu ya Taifa, ameeleza kuwa mwaka huu kulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuingiza wachezaji bora, hivyo nafasi walitopata waogeleaji wake wamejitahidi.

Kuhusu nafasi ya Tanzania katika mchezo huo kocha huyo  amesema inazidi kupanda kutokana na ushirikiano wanaopewa na Serikali pamoja na wazazi, hivyo kuomba kuzidi kuimarisha hali hiyo ili kufikia viwango vya juu zaidi.

Kwa upande wa kocha wa timu ya Bandari, Fakhry Mansoor, amesema  wao wamelikwa na wamekaribishwa vizuri hadi wamefurahia lakini kiushindani Tanzania inazidi kupiga hatua, hali inayowafanya wakirejea nyumbani wakafanye kazi kubwa kurejesha ubora wao.

“Kwa kweli miaka ya nyuma kidogo ilikuwa tukikutana na Tanzania katika mashindano ya kuogelea tulikuwa tukiwachafua lakini sasa hivi wao wanatuchafua. Kwa kweli tumepata mshangao mkubwa Tanzania ina maendeleo makubwa na viongozi wanafanya kazi nzuri,” ameeleza kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles