27.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kiwanda cha TPC kinavyosaidia Jamii Kilimanjaro

Na Safina Sarwatt, Moshi

Kiwanda cha Sukari TPC kilichopo Kata ya Arusha chini wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kimeanzisha mpango maalumu wa kuziboresha shule nne za msingi zilizopo kwenye vijji vinavyozunguka kiwanda hicho kwa kuzifanyia ukarabati wa madarasa pamoja ujenzi wa majengo mapya.

Miongoni mwa shule zilizofanyiwa ukarabati ni shule ya msingi Mikocheni ambayo ukarabati wake umegharimu Sh milion 200 na shule ya msingi Kiyungi ambayo ukarabati wake umegharimu Sh milioni 56.

Pia TPC imetenga Sh milioni 60 kwa ajili ya kumalizia ukarabati wa shule za Sekondari na Msingi Arusha chini ikikarabatiwa kwa gharama ya Sh millioni 200.

Kwa upande wa shule za sekondari TPC imejenga shule mpya ya Sekondari ya Chekereni Weruweru ambayo itakuwa Mwarobaini kwa wanafunzi zaidi ya 600 waliokuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu w kilometa 27 kwenda na kurudi kusaka elimu.

Kujengwa kwa shule hiyo bi hatua kubwa kwa wanafunzi pamoja na wazazi kwani itapunguza changamoto nyingi zilizokuwepo ikiwamo utoro pamoja na kuongeza ufaulu kutokana na wanafunzi hao kusoma katika mazingira rafiki kwani .

Kabla ya kujengwa kwa shule hiyo wanafunzi hao walikuwa wanasoma shule ya sekondari ya TPC umbali wa zaidi ya kilometa 10 kutoka Chekereni ya Weruweru huku baadhi wakikatisha masomo kutokana na changamoto hiyo ya umbali wa eneo la kusomea hususan wasichana.

TPC kupitia Taaisis ya mradi FTK imeweza kukusanya fedha na kutenga zaidi ya Sh billioni 1.4 kwa mwaka asilimia kubwa ya fedha hizo zimelekezwa kwenye sekta ya elimu ikiwamo kukarabati shule za msingi na sekondari zinazozunguka kiwanda hicho ikiwa ni mkakati wa kiwanda hicho kuboresha mahusiano na jamii inayowazunguka.

Afisa Mtendaji wa kiwanda hicho anayeshughulikia masuala ya utawala, Jafary Ally amesema mkakati wa TPC ni kujenga mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi pamoja na Serikali Kuu.

Amesema kiwanda hicho sambamba na uzalishaji wa sukari imeweka mikakati mbalimbali ya kusaidia jamii inayoizunguka ikiwamo uboreshaji wa elimu kwa shule za awali msingi na sekondari lengo ni kuimerisha ujirani mwema.

Amesema hivi karibu wanatenga shule mpya ya sekondari ya Chekereni Weruweru kutokana na wanafunzi kutoka umbli mrefu kilometa 27 kuja kusoma shule ya sekondari TPC.

Anasema shule hiyo imesaidi wanafunzi zaidi ya 600 ambao walikuwa wakiteseka kufuata huduma ya elimu.

Anafafanua zaidi kuwa wanafunzi hao kwasasa wanapata huduma bora ya elimu katika shule na mazigira bora kwa ukaribu zaidi.

Kiwanda hicho kupitia kupitia Taasisi yake ya FTK wanafadhili wanafunzi 250 kusoma vyuo vya ufundi na vyuo vikuu kila mwaka, bila kuchangia gharama zozote na bila masharti kwamba wakimaliza masomo yao wakafanye kazi TPC.

“Wapo wanafunzi wanaoomba mikopo bodi ya mikopo na kupewa pengine asilimia 60, sisi TPC tunajazia aslimia iliyobaki na tunafanya hayo yote tukiamini kwamba ukisaidi jamii umelikomboa Taifa kiuchumi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles