26.1 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Mashindano ya Taifa ya klabu kuogelea yaanza kwa kishindo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mashindano ya Taifa Klabu ya Kuogelea yameanza leo Aprili 20,2024, huku  waogeleaji kutoka klabu mbalimbali wakionekana kuchuana vikali  kwenye bwawa la kuogelea  la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika(IST), Masaki jijini Dar es Salaam.

Michuano  inayotarajiwa kumalizika kesho Aprili 21,2024 inashirikisha jumla ya  klabu 11 za Tanzania na mbili zikitokea nchini Kenya.

Akizungumzia  mwanzo wa mashindano hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania(TSA),David Mwasyoge, amesema mashindano hayo yana ushindani mkubwa kwa sababu washiriki  ni wale waliofikia vigezo  vya dunia.

“Mashindano haya klabu zimepungua  na hata washiriki ni wachache kwa sababu yana ushindani wa hali ya juu na  ilikuwa ili uweze kushiriki lazima ufikie vigezo vya dunia,”amesema.

Ameeleza kuwa mikakati ya chama ni kuhakikisha  vijana wengi wa Kitanzania wanashiriki katika mchezo wa kuogelea na kuondoa dhana kuwa mchezo huo ni wa matajiri.

“Tanzania ina vipaji vingi vya kuogela na tumegundua watoto wengi wanapenda maji, sababu ukiangalia kwenye sherehe nyingi wazazi wanawapeleka  watoto wao kwenda kuogelea, kwa hiyo lengo letu ni kuwapa mafunzo,” amesema.

Kwa upande wake muogeleaji  Crissa Dillip,  amesema mashindano ni magumu kutokana na ushindani uliopo lakini anaamini atafanya vizuri na kuwa miongoni mwa wachezaji bora wa michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles