22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya NBC Yazindua Huduma Maalum Kuwashika mkono Wastaafu

Na Mwandishi Wetu

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa ajili ya wastaafu inayofahamika kama “Akaunti ya Wastaafu” ama “Pensioners account” ikilenga kutoa huduma za kibenki zenye kutoa vipaumbele kwa kundi hilo la kijamii.

Kupitia huduma hiyo iliyozinduliwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam,  pamoja na faida nyingine  inatoa fursa ya mikopo mikubwa hadi milioni 300 kwa wastaafu, itakayolipwa kwa kipindi cha miaka 9 huku walengwa wakinufaika na ushauri wa kifedha na elimu ili kuwajengea maarifa na rasilimali wanazohitaji kufanya maamuzi sahihi kuhusu fedha zao na malengo yao ya kifedha.

Akiizungumzia zaidi huduma hiyo, Mkuu wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki hiyo, Elibariki Masuke alisema imeangazia zaidi  katika kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali za huduma za kifedha zinazokabili wastaafu nchini huku ikitoa mwanga wa kesho bora kwa kundi hilo kupitia upendeleo maalum wa kihuduma.

Meneja  Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea Mabonye (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu huduma ya mpya maalum kwa ajili ya wastaafu inayofahamika kama “Akaunti ya Wastaafu” Wengine ni Mkuu wa Idara ya Wateja wadogo na Wakubwa wa benki ya NBC, Elibariki Masuke (kulia) na Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani Bi Zubeider Haroun (Kushoto).

“NBC imeamua kumuangalia kipekee mstaafu kwa sababu tunaelewa umuhimu wa kipindi cha kustaafu. Kustaafu sio tu mwisho wa kazi, ni mwanzo wa sura mpya yenye uhuru wa kifedha na usalama. Ni wakati ambapo tunapaswa kuhakikisha kwamba wastaafu wetu wanapata huduma za kifedha zilizoboreshwa ambazo zitawawezesha kustawi kifedha.’’

‘’Tunatambua changamoto ambazo wastaafu wanakabiliana nazo, na ndio maana NBC tumechukua hatua za kuboresha  huduma zetu za kibenki ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu walio katika makundi mbali mbali ya mahitaji.’’ Alisema.

Zaidi alitaja faida nyingine zinazoambatana na akaunti hiyo kuwa ni pamoja na kutokuwa na makato ya ada ya kila mwezi huku upatikanaji wake ukirahisishwa kidigitali kwa njia ya simu yaani NBC Kiganjani, na pia kupitia msaada  binafsi kutoka kwa wataalamu wa benki hiyo.

Akizungumzia mafunzo na elimu ya fedha kwa wastaafu, Meneja  Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea Mabonye alisema benki hiyo Imekuwa ikishirikiana na taasisi za kijamii na mashirika yanayotoa huduma kwa wastaafu ikiwemo mifuko ya kijamii kama vile PSSSF na NSSF kutoa elimu ya kifedha kwa wanachama wao wanaotarajia kustaafu ndani ya muda mfupi ujao.

“Lengo letu ni kuongeza matumaini na furaha kwa wateja wetu hata pindi wanapostaafu. Tunataka kuhakikisha kwamba miaka ya baadaye ya wateja wastaafu wanakuwa na amani na furaha bila wasiwasi wa kifedha.’’ Aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles