25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wataalamu 52 kutoka Taasisi za Fedha wapigwa msasa namna bora ya kutoa mikopo ya Kilimo

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) imefunga mafunzo kwa wataalam 52 kutoka Benki washirika kuhusu namna bora kutoa mikopo katika sekta ya kilimo na kuangalia viatarishi jambo ambalo litasaidia taasisi za fedha nchini kufanyakazi kwa ufanisi na kuleta tija kwa Taifa.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) DktEphraim Mwasanguti, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka Benki washirika kuhusu namna bora ya kutoa mikopo katika sekta ya kilimo.

Mafunzo hayo yameendeshwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kupitia BoT Academy kwa lengo la kuzalisha wataalam wengi katika taasisi za fedha ambao watasaidia kutoa mikopo.

Akizungumza Mei 3, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi na Muendeshaji wa TADB, Dk. Kanael Nnko, amesema mafunzo hayo yanakwenda kuleta tija katika utoaji wa mikopo sekta ya kilimo.

“Tunaamini mafunzo haya pamoja na washiriki yanakwenda kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yetu ya hakikisha sekta ya kilimo inasonga mbele,” amesema Dk. Nnko.

Amesema lengo la mafunzo  hayo ni kuwa na wataalam  ambao watasaidia kutoa mikopo katika sekta nzima  ya kilimo naKuhakikisha idadi kubwa ya wakulima wanafikiwa na kupata mikopo katika Mikoa yote kwa maendeleo ya Taifa.

Amesema kuwa TADB katika kipindi cha miaka sita hadi sasa mfuko wa dhamana Benki ya kilimo. imeweza kudhamini mikopo ya shilingi bilioni 270 kupitia benki washirika.

Amesema kuwa TADB katika kipindi cha miaka sita hadi sasa mfuko wa dhamana Benki ya kilimo. imeweza kudhamini mikopo ya shilingi bilioni 270 kupitia benki washirika.

Ameeleza kuwa wameweza kuwafikia wakulima walengwa 24,000, huku benki ya washirika wametoa asilimia 11 ya mkopo katika sekta ya kilimo na kuendelea kuongeza juhudi ili kufikia mwaka 2030 sekta ya mikopo imefikia  asilimia 30 ya malengo.

“Kilimo ni sekta kubwa hivyo huwezi kuwafikia wote kwa siku moja, juhudi zinaendelea kufanyika ili vijana, wakina mama na baba waweze kuingia katika sekta ya kilimo,” amesema.

Kwa upande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Ephraim Mwasanguti, amesema kuwa miongoni mwa majukumu yao ni kutoa elimu kwa mabenki na taasisi za fedha kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

“Tulipewa kazi na benki ya maendeleo ya kilimo ya kutengeneza programu kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo hasa ikilenga kuelimisha mabenki hasa maafisa mikopo ili waweze kutoa mikopo ambayo italipika kwa sababu hizi ni fedha za umma na kuleta matokeo mazuri katika nchi yetu,” amesema Dk. Mwasanguti.

Dk. Nnko amefafanua kuwa mafunzo hayo yameendeshwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia BoT Academy pamoja na washirika wengine kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) ambao wameshiriki katika kuunda mifumo pamoja na kufundisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles