26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Cobhams Ssuquo agonga kolabo na Sauti Sol kwenye video “Lady Fiona”

Na Joseph Shaluwa, Mtanzania Digital

MSANII maarufu nchini Nigeria, Cobhams Asuquo ameshirikiana na kundi maarufu nchini Kenya, Sauti Sol kwenye video inayokwenda kwa jina la ‘Lady Fiona’.

Cobhas ambaye pia ni mwandishi wa mashairi na mtayarishaji muziki nchini humo, ameunganisha nguvu na miamba ya muziki nchini Kenya, Sauti Sol ambao wameshikilia tuzo ya kundi bora la muziki wa Afro-Pop, Kenya.

Huu ni ushirikiano mzuri wa kimataifa unaowakutanisha miamba ya muziki barani Afrika na kuunganisha pamoja sauti zao tamu zinazotoa burudani ya aina yake kwa hadhira.

“Lady Fiona” ni wimbo wa aina yake wenye mahadhi ya Afro-pop, unaotoa nafasi ya ubunifu wa wasanii hawa – Cobhams Asuquo na Sauti Sol,” inaeleza sehemu ya taarifa kwa vyombo vya habari.

Ni wimbo unaowafanya wasikilizaji wazame katika ulimwengu wa mahaba na kuibua hisia zinazoweza kumpata mtu yeyote ambaye amepitia furaha au magumu katika mahusiano ya kimapenzi.

“Ombi letu kubwa kwa mashabiki wa muziki mzuri ni kuitazama video hiyo ambayo tayari inapatikana mitandaoni. Hapo ukweli wa haya tunayosema utathibitika,” ilihitimisha taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles