26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Dulla Mbabe kusapoti mabingwa wa Kusini kesho

NA MWANDISHI WETU, Mtanzania Digital

MABONDIA kutoka Wilaya za mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara wanatarajia kupanda ulingoni kesho katika mapambano ya kusaka mabingwa wa Kusini kwenye ukumbi wa Iwawa, Masasi.

Miongoni mwa mabondia hao ni kutoka Wilaya za Tandahimba, Masasi na Mtwara, huku bondia maarufu nchini Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’, akitarajia kusindikiza.

Mabondia watakaopatikana katika mchuano huo, watapata nafasi ya kupigana kwenye pambano la Seleman Kidunda dhidi ya Tshimanga Katompa kutoka DR Congo, Julai 30,2022 mwaka huu, Songea mkoani Ruvuma.

Akizungumzia mapambano hayo, kocha wa ngumi mikoa ya Kusini, Bashiru Selemani, amesema hiyo ni nafasi kwao kuonyesha uwezo na vipaji vya mabondia wao.

“Mashabiki wa ngumi Tanzania wajue kuwa tunao mabondia wenye uwezo hali ya juu wa uzito tofauti, hivyo tuko tayari kumpiga bondia yeyote atakayekuja,” ametamba kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles