21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

InstaUnited FC yazindua jezi, GF Trucks yajitosa

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital
KUELEKEA msimu mpya wa michuano ya Ndondo Cup 2022, timu mpya ya InstaUnited imepata udhamini wa Kampuni ya Uuzaji na Utengenezaji wa magari makubwa ya GF Trucks katika kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vizuri.

Pamoja na udhamini huo, InstaUnited imezindua jezi za nyumbani na ugenini itakazotumia msimu, ikiwamo wimbo wa uhamasishaji wa timu hiyo.

Hafla ya kutangaza udhamini huo na uzinduzi wa jezi hizo ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Meya wa Dar es Salaam, Saad Khimji, ilifanyika leo Mei 5, 2022 kwenye ofisi za GF Trucks, zilizopo Vingunguti.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Chiku Said, amesema lengo la timu hiyo ni kuinua vipaji vya vijana, hivyo wanahitaji uwekezaji ili kufanikisha malengo yao.

“Kama klabu inahitaji uwekezaji, hivyo leo tunatangaza kampuni ya GF Trucks kuwa mwanafamilia wetu wa kutushika mkono kuelekea Ndondo Cup 2022 kwa kuwa tunahitaji kuwafikia vijana wengi,” amesema Chiku.

Naye Mkurugenzi wa GF Trucks, Ali Karmali, ameeleza kuwa muunganiko pande hizo mbili na kilichowavutia ni kutokana na timu hiyo kusapoti vijana, hivyo anaamini watatangazika vizuri.

“Tumeamua kuishika mkono timu ya InstaUnited kwa sababu ni timu ya vijana na ina ushirikiano mkubwa na waandishi wa habari watatutangaza vizuri kutokana na hamasa iliyoanza,” amesema Karmali.

Kwa upande wake Naibu Meya Khimji, ameipongeza timu hiyo kwa hatua ilifikia na kasi waliyoanza nayo, akiamini kuwa ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ndondo Cup.

“Mimi ni mdau wa michezo na nimekuwa nikifuatilia mashindano haya tangu yalipoanza, lakini hii ni mara ya kwanza kuona jambo kama hili linafanywa na timu inayoshiriki Ndondo Cup,” ameeleza Khimji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles