29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Makete achangia mjadala mfumuko bei ya mafuta

NA MWANDISHI WETU, Mtanzania Digital

MBUNGE wa Jimbo la Makete, Festo Sanga amesimama Bungeni kuchangia mjadala wa mfumuko wa bei ya mafuta na kusema suala hilo si dogo litaathiri maisha ya watu.

“Bei ya mafuta duniani hadi yanafika Dar es Salaam ni Tsh 1,162 kwa lita lakini msalaba na mnyororo wa kodi na tozo ni zaidi ya 1,300, yaani bei ya mafuta duniani ni ndogo kuliko mnyororo wa kodi tulizonazo, mimi niombe Serikali kuona umuhimu wa kupunguza hizi kodi.

“Suala la mafuta sio jambo dogo, ni jambo kubwa ambalo linaathiri kuanzia maisha ya mtu wa chini kabisa hadi wa mwisho, niwaombe Serikali hata kama tupo kwenye mazungumzo kwenye vikao tunavyoendelea navyo hili jambo ni la dharura lazima tulichukue katika udharura wake.

“Tozo ni nyingi sana, zipunguzwe kwa udharula tulio nao ili kunusuru msalaba wa ugumu wa maisha ya Watanzania hivi sasa. Serikali itafute fedha mahali pengine kwa ajili ya kuweka ruzuku kwenye mafuta ili bei ishuke.

“Hali ya maisha imekuwa ngumu, mafuta yanamnyororo mrefu kwenye bidhaa na huduma mbalimbali. Yanapopanda yaaathiri kila sekta ya kiuchumi,” amechangia Sanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles