CALIFORNIA, MAREKANI
BABA wa staa wa zamani wa muziki wa Pop, Michael Jackson, Joe Jackson, anadaiwa kuzikwa kwa siri katika misitu ya Lawn Memoriol Park, California nchini Marekani.
Inasemekana kuwa mazishi hayo yalifanyika juzi huku baadhi ya wanafamilia wa marehemu wakihudhuria na ndugu wengine wakitakiwa kwenda siku inayofuata kushuhudia kaburi.
Miongoni mwa watu waliokuwepo kwenye mazishi hayo ni pamoja na aliyekuwa mke wa Michael Jackson, Katherine pamoja na watoto wake nane wakiungana na Janet Jackson.
Joe Jackson alipoteza maisha wiki iliyopita nyumbani kwake Las Vegas, Nevada, huku akiwa na umri wa miaka 89, baada ya kusumbuliwa na saratani ya kongosho ya hatua ya mwisho.