28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

JAPAN WAACHA HISTORIA KOMBE LA DUNIA


ROSTOV-ON-DON, URUSI


TIMU ya Taifa ya Japan imeacha historia kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, baada ya kutolewa katika hatua ya 16 bora dhidi ya wapinzani wao Ubelgiji kwa mabao 3-2, kwenye Uwanja wa Rostov.

Wasimamizi wa michuano hiyo wameshangazwa na timu hiyo baada ya kufanya usafi katika chumba chao cha kubadilishia nguo, ikiwa ni dakika chache baada ya kufungashiwa virago dhidi ya wapinzani wao.

Msimamizi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Priscilla Janssens, ameweka wazi kuwa hakutarajia kuona kilichofanywa na wachezaji wa timu hiyo, ikiwa baadhi yao walitoka uwanjani huku wakitokwa na machozi kutokana na kuondolewa kwenye michuano hiyo.

“Tunaweza kusema Japan ni timu ya kuigwa, wameposti picha kwenye mtandao wao wakionesha chumba chao cha kubadilishia nguo kikiwa safi baada ya dakika 90 kumalizika na waliandika ‘hiki ni chumba cha wachezaji wa Japan baada ya kufungwa dhidi ya Ubelgiji.

“Hata hivyo, waliwashukuru mashabiki wao kwa sapoti uwanjani hapo, pia waliacha ujumbe kwenye ukumbi wa mikutano na waandishi wa habari ambao uliandikwa ‘Asanteni Urusi’ hii ni timu ya mfano wa kuigwa,” alisema Janssens.

Kwa hali ya kawaida, timu ikiwa imetolewa inakuwa kwenye wakati mgumu na si rahisi kufanya usafi hata kama timu imeshinda, lakini Japan wameshangaza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,085FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles