23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

FORSBERG AIPELEKA SWEDEN ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

SAINT-PETERSBURG, URUSI


KIUNGO wa timu ya taifa ya Sweden, Emil Forsberg, amefanikiwa kuipeleka timu hiyo hatua ya robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, baada ya kufunga bao lake katika dakika ya 66.

Sweden imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwachapa wapinzani wao Switzerland bao 1-0.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza hazikuwa na ushindani sana huku kila timu ikifanya mashambulizi ya kushtukiza, hivyo dakika hizo zilimalizika bila ya nyavu kutikisika.

Sweden ilikuwa inatumia mfumo wa 4-4-2, wakati huo wapinzani wao wakitumia 4-2-3-1, lakini Sweden walionekana kumiliki mpira katika eneo la katikati.

Dakika 45 za kipindi cha pili, Sweden walionekana kutafuta bao, walifanya mashambulizi ya mara kwa mara kupitia kwa washambuliaji wao wa pembeni kama vile Martin Olsson mwenye asili ya Kenya, hivyo mashambulizi hayo yalionekana kuwa na hatari tangu dakika ya 61, ila walikuja kupata bao hilo dakika ya 66 kutokana na pasi iliyopigwa na Ola Toivonen.

Bao hilo liliufanya mchezo huo kuwa wazi, huku Switzerland wakipambana kuhakikisha wanapata bao la kusawazisha, lakini walinzi wa Sweden walionekana kuwa imara katika dakika 15 za mwisho, huku wakihakikisha wanaondoa mipira yote ya hatari.

Mbali na Switzerland kupambana kuhakikisha wanapata bao la kusawazisha, lakini Sweden walifanya shambulizi dakika za mwisho na kupata mpira wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari, baada ya Olsson kuchezewa vibaya na beki wa Switzerland, Michael Lang.

Hata hivyo, wachezaji wa Sweden waliamini kuwa watapata mkwaju wa penalti, lakini kutokana na uchunguzi wa mtambo wa VAR, iligundulika kuwa si penalti, hivyo mpira huo wa adhabu ulipigwa na kuokolewa. Mpira ulimalizika na kuwafanya Sweden kufuzu hatua ya robo fainali na kumsubiri mshindi kati ya Colombia dhidi ya England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles