Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe, ametaka Bunge kuahirisha shuguli zake leo na kujadili tatizo la utekaji watu alilosema linaharibu sifa ya nchi. Amesema pia amepewa taarifa kwamba yupo kwenye kundi la wabunge 11 ambao wamewekwa kwenye orodha ya wabunge wanaotaka kuuliwa na kikundi hicho wakikaa vibaya barabarani.