28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

ROMA, WENZAKE KUSIMULIA KUTEKWA KWAO LEO

Na WAANDISHI WETU


RAPA Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ na wenzake watatu, leo wanatarajiwa kueleza sakata zima la tukio la kutekwa kwao wakiwa studio za Tongwe Records Masaki, jijini Dar es Salaam.

Wasanii wanaodaiwa kutekwa ambao wataungana na Roma katika mkutano na waandishi wa habari leo ni Moni Centrozone, prodyuza wa studio hiyo, Bin Laden na mfanyakazi wa mama mzazi wa mmiliki wa studio hiyo, Junior Makame (J Murder), anayefahamika kwa jina la Imma.

Juzi usiku baada ya kuruhusiwa kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam na kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Mwananyamala, Roma aliwaambia waandishi wa habari kwamba atazungumza leo.

“Mi ni mzima kabisa, nipo vyema kiafya na kiakili na wenzangu watatu nikimaanisha Mon, Bin Laden prodyuza wetu pamoja na Imma mfanyakazi wetu pale Tongwe; wote tu wazima tunaendelea vizuri, kwa sasa tupo katika taratibu za kutoa taarifa za tukio zima ambavyo limetokea.

“Lakini taratibu hizo zinatufunga tusiweze kuongea chochote kwa sasa hivi, lakini ratiba naweza kuwapa kushinda kesho Jumapili, Jumatatu nadhani ndiyo kutakuwa na ‘Press Conference’ kukutana na kuongelea kuhusu hiyo stori, mturuhusu tu tukapumzike nawashukuru, niseme tu asante,” alisema Roma.   

Roma na wenzake walitekwa Jumatano wiki hii wakiwa katika studio za Tongwe Recods iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Chama cha muziki

Katika hatua nyingine, pia Chama cha Muziki wa Kizazi kipya (TUMA) nacho kinajipanga kutoa tamko lao kuhusiana na utekwaji huo baada ya Roma kuelezea umma kilichotokea.

Katibu Mkuu wa TUMA, Samwel Mbwana ‘Brayton’, aliliambia MTANZANIA kwamba licha ya kutoa tamko hilo pia watatoa elimu na tahadhari kwa wasanii kuepuka migogoro itakayowasababishia kuingia katika matatizo kama yaliyowatokea wasanii wenzao.

“Tutaweka mipaka katika uhuru wa kuongea na kuwa makini kama alivyosema Rais John Magufuli na pia tutaimarisha umoja wetu katika malengo chanya na si kwa matatizo pekee,” alisema Brayton.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles