23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Watu 28 wafungwa jela kwa kughushi vitambulisho

RABAT, MOROCCO

MAHAKAMA ya Morocco imewafunga jela watu 28 baada ya kuwatia hatiani kwa kughushi na kutoa nyaraka bandia kwa ajili ya kutengenezewa vitambulisho vya uraia, Wazayuni.

Mahakama ya rufaa ya Morocco siku ya Alhamisi iliendelea kufuatilia kesi za watuhumiwa hao 28 waliokula njama za kuwapa vitambulisho vya uraia Waisrael kinyume cha sheria.

Mahakama hiyo imewahukumu kifungo cha miaka sita jela watuhumiwa watatu wakuu akiwemo mkuu wa genge hilo ambaye yeye mwenyewe ni Myahudi pamoja na wanawake wengine wawili.

Vyombo vya habari vimetangaza kuwa: “Hatimaye mahakama ya rufaa ya Morocco imelipata genge hilo, na hatia ya kughushi na kutoa vyeti bandia kwa raia wa utawala wa Israel.”

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa al Khalij al Jadid, mahakama hiyo ya Morocco imewatia hatiani pia watu wengine watatu akiwemo Myahudi mmoja na kuwahukumu kifungo cha miaka minne jela kila mmoja.

Watuhumiwa wengine waliobakia wamepewa adhabu tofauti na ahakama hiyo.

Katika safu ya watuhumiwa hao wamo pia maofisa watatu wa polisi na mkuu wa shirika moja la usafiri la Morocco.

Machi mwaka huu, maofisa wa Morocco walitangaa kuwa, wamewatia mbaroni watu 28 kwa tuhuma za kutengeneza vitambulisho na vyeti bandia kwa ajili ya walowezi wa Kiyahudi.

Wanane kati ya watu hao ni walowezi wa Kiyahudi.

Hata hivyo sehemu kubwa ya watu hao ni raia wa Morocco na uchunguzi unaonesha kuwa walijipenyeza katika taasisi za usalama na zile zinazohusiana na vyeti na nyaraka na kufanya uhalifu huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles