22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

UN: Haki za binadamu zimeporomoka

NEW YORK, MAREKANI

MUONGO mmoja uliopita umeshuhudia kurejea nyuma kwa haki za binadamu katika kila sehemu, hususan haki kwa wanawake. Ofisa wa Umoja wa Mataifa (UN) anayehusika na masuala ya haki za binadamu, Andrew Gilmour, alisema kuporomoka huko katika miaka 10 iliyopita kunalingana na hatua zilizopigwa ambazo zilianza katika miaka ya mwisho ya 1970, lakini hali hiyo imefikia kiwango kibaya, kusambaa kila mahali na inasikitisha.

Katibu mkuu huyo msaidizi anayeondoka madarakani, alizungumzia kuhusu siasa za kizalendo za kimabavu, Kaskazini mwa Amerika, Kusini mwa Amerika, Ulaya na Asia, ambako alisema wanawalenga makundi ya wachache wasio na uwezo katika jamii.

Alisema makundi hayo ni yale ya Waislamu wa Rohingya wa Myanmar, Waroma, wahamiaji wa Mexico, pamoja na wanawake.

Alidokeza kuhusu viongozi ambao wanaunga mkono utesaji, kukamatwa na kuuawa kwa waandishi habari, ukandamizaji wa kinyama wa waandamanaji na kufunga kwa nafasi y

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles