25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mlipuko wa bomu waua watu 76 Somalia

MOGADISHU, SOMALIA

TAKRIBANI watu 76 wamedaiwa kufariki kufuatia mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari wakati wa pilika pilika nyingi katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

Mlipuko huo ulitokea katika kituo kimoja cha kukagua magari katika eneo la makutano ya barabara mjini Mogadishu.

“Mlipuko huo ulikuwa mbaya mno na naweza kuthibitisha kwamba zaidi ya raia 20 waliuawa, huku wengine wengi wakijeruhiwa,” ofisa wa Polisi, Ibrahim Mohamed alinukuliwa na kituo cha habari cha AFP akisema.

Hakuna kundi ambalo limekiri kutekekeleza kitendo hicho lakini wapiganaji wa kundi la al- Shabab wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara katika taifa hilo.

Al-Shabab, kundi la wapiganaji, linaloshirikiana na kundi la kigaidi la Al-

Qaeda limekuwa likitekeleza mashambulizi kwa zaidi ya miaka 10.
Kundi hilo lilifurushwa kutoka mji mkuu wa Mogadishu mwaka 2011 lakini linadhibiti baadhi ya maeneo ya taifa hilo.

Walioshuhudia walielezea kilichotokea katika eneo la mkasa huo.

“Kile ambacho niliweza kuona ni watu waliofariki…wakati wa mlipuko huo huku baadhi yao wakichomeka, hkwa kiwango cha kutoweza kutambulika,” alisema Sakariye Abdulkadir, ambaye alikuwa karibu na mlipuko huo.

Mbunge mmoja wa Somalia, Mohamed Abdirizak, alisema kuwa idadi ya watu waliofariki dunia ni zaidi ya 90, ijapokuwa habari hiyo aliyopata anasema kwamba haijathibitishwa.

“Mungu awarehemu waathiriwa wa shambulio hili la kikatili,” aliongezea waziri huyo wa zamani wa usalama wa ndani.

Watu watano waliuawa mwezi huu wakati wapiganaji wa Alshabab waliposhambulia hoteli moja ya Mogadishu inayopendwa sana na wanasiasa, wanadiplomasia na wanajeshi.

Mkuu wa hospitali ya Medina, Mohamed Yusuf alithibitisha idadi hiyo akisema watu wengine 70 wamerujiwa.

Awali, msemaji wa Serikali, Ismail Mukhtar alisema idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu zaidi ya watu 60 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali.

Limekuwa mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi kutokea katika siku za karibuni mjini Mogadishu.

Kapteni Mohamed Hussein alisema mlipuko huo ulikilenga kituo cha kukusanya kodi wakati wa pilikapilika za asubuhi wakati wakazi wakirejea kazini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa juma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles