26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi yazindua mfumo mpya wa kombora

MOSCOW, URUSI

Russia yazindua mfumo mpya wa kombora lenye kasi zaidi ya sauti la ‘Avangard Hypersonic’.

Shirika la Habari la Itar-Tass la Russia liliripoti kwamba Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Sergey Shoygu, alizindua mfumo wa kwanza wa makombora ulio na kasi kubwa kuliko sauti juzi Ijumaa.

Kwa mujibu wa shirika hilo la habari, shughuli ya uzinduzi wa mfumo huo, ilifanyika majira ya saa 10 asubuhi kwa majira ya

Moscow, mji mkuu wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo Jumamosi iliyopita pia, Rais Vladmir Putin wa Urusi na katika kikao kilichohudhuriwa
na maofisa wa ngazi za juu wa jeshi la nchi hiyo, akiwemo Sergey Shoygu, Waziri wa Ulinzi, alisema uzinduzi huo ni w akihistoria.

Alisema kuwa kinyume na huko nyuma katika harakati za ushindani na Marekani, kwa mara ya kwanza katika historia yake, Russia imefikia kiwango cha juu katika uundaji wa zana mpya za kivita.

Akibainisha suala hilo, Putin alisema: “Tumefikia kiwango cha uwezo wa kijeshi cha zama hizi, na hivi sasa ni Marekani inayopigania kuweza kutufikia. Hakuka nchini yenye silaha za Hypersonic, achilia mbali silaha za Hypersonic za kuvuka mabara.”

Akizungumzia makombora ya Avangard hypersonic alisema kuwa, makombora hayo ya kuvuka mabara yanaweza kwenda umbali wa anga ya dunia kwa kasi ya mara 20 zaidi ya sauti sambamba na kuvuka aina yoyote ya ngao ya kiulinzi iliyopo duniani.

Akiashiria suala la kuongeza askari kunakofanywa na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) katika mipaka ya Magharibi mwa Urusi, na kitendo cha Marekani cha kujiondoa kwenye mapatano ya makombora ya masafa ya wastani yaliyotiwa saini mwaka 1987, Rais Putin alisema ni lazima Urusi imiliki silaha za kisasa duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles