24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAISLAMU WALAANI MARUFUKU YA HIJABU KATIKA MAHAKAMA YA EU

MUNICH, UJERUMANI


WAISLAMU barani Ulaya wamelaani vikali hatua ya Mahakama ya Uadilifu ya Ulaya kutoa hukumu kuwa waajiri wanaweza kuwazuia wafanyakazi wa kike Waislamu kuvaa hijabu kazini.

Nchini Ujerumani, Baraza Kuu la Waislamu limekosoa vikali hukumu hiyo likisema inakiuka haki za kimsingi ambazo zimeainishwa katika mikataba muhimu ya Ulaya kuhusu haki za binadamu.

Naye Bekir Altas, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Milli Gorus, inayowakutanisha pamoja Waislamu wenye asili ya Uturuki huko Ujerumani, amelaani hukumu hiyo.

Mahakama ya Haki ya Ulaya (ECJ) yenye makao yake huko Luxembourg Jumanne iliyopita ilipasisha marufuku ya vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu (Hijab).

Kwa mujibu wa hukumu ya mahakama hiyo, waajiri wa Ulaya wanaweza kuwazuia wafanyakazi wao kuvaa nembo za kidini likiwemo vazi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles