25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI YAONGOZA KWA KUWA NA WAFUNGWA WENGI DUNIANI

RIPOTI mpya iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa idadi ya wafungwa wanaoshikiliwa katika jela za Marekani ni kubwa zaidi kuliko ya nchi zote duniani.

Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya "Policy Think Tank  imeonyesha kuwa hivi sasa karibu wafungwa milioni 2.3 wapo katika jela za nchi hiyo.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa idadi ya wafungwa walioko katika jela za Marekani ni mara tano zaidi ya idadi ya wafungwa wa nchi zenye wafungwa wengi duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kati ya kila wafungwa watano walioko jela, mfungwa mmoja amehukumiwa kifungo jela kwa kosa linalohusiana na madawa ya kulevya. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa kuna haja ya kutazamwa upya sera ya kuendesha mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili kupunguza idadi kubwa wafungwa nchini Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles