27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AMSHANGAA MWAKYEMBE, ATOA RUKSA KUOANA BILA CHETI CHA KUZALIWA

RAIS John Magufuli amelifuta agizo la watu kutofungishwa ndoa kwa watu wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa kuanzia Mei mwaka huu, lililotolewa jana tarehe na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe.

Aidha, amewatoa hofu Watanzania na kuwataka kuendelea na utaratibu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe basi atamuelekeza Dk. Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma leo, Rais Magufuli amesema serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.

“Hadi sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961,” amesema.

Hata hivyo, Rais Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi ambapo pia ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.

Dk. Mwakyembe akiwa ziarani mkoani Morogoro jana, alisema kuanzia Mei mosi mwaka huu watu hawataruhusiwa kuoana bila kuwa na vyeti vya kuzaliwa na kwamba serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles