24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji gofu kuchuana Johnnie Walker Waitara Trophy Januari 29

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

MASHINDANO ya Johnnie Walker Waitara Trophy 2021, yanatarajia kutimua vumbi Januari 29,2022, yakishirikisha wachezaji wa ridhaa na kulipwa kutoka klabu mbalimbali Tanzania.

Michuano hiyo ambayo ambayo ni ya kwanza mwaka huu itafanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Januari 21,2022, Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo,Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, amesema michuano hiyo ilitakiwa kufanyika mwaka jana, lengo ni heshima ya muasisi wa klabu hiyo, Jenerali George Waitara.

Amesema kuwa mashindano hayo hufanyika kila mwaka, huku akitaja baadhi ya klabu shiriki kuwa ni Moshi, Arusha Gymkhana, Mufindi Klabu,Morogoro Gymkhana,Dar es Salaam Gymkhana,Sea Cliff Golf klabu Zanzibar, Kili Golf na TPC Golf klabu.

Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo,Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo(kushoto), akipokea kombe litakalotolewa zawadi katika mashindano hayo kutoka kwa Meneja Masoko wa Serengeti Lumuli Minga.

Ameongeza kuwa mwitiko wa wachezaji kujisajili ni mkubwa ambapo hadi sasa wamefikia 100 na usajili unatafungwa Alhamisi asubuhi.

“Maandalizi yanakwenda vizuri tuna uwezo wa kupokea idadi ya wachezaji wowote, watu waendelee kujisajili,” amesema.

Aidha amesema nafasi ya watoto haitakuwepo kwa sababu ya wadhamini wao ni wa kileo hivyo ni kinyume na malezi ya watoto.

Kwa upande wake nahodha wa klabu hiyo, Meja Japhet Masai, amesema kuwa mashindano hayo ni ya siku moja ambapo itaanza na shindano la wachezaji wa kulipwa Ijumaa.

Nahodha wa Klabu ya Gofu Lugalo, Meja Japhet Masai, akizungumzia maandalizi ya Johnnie Walker Waitara Trophy mbele ya waandishi wa habaro leo Januari 21,2022

Amesema wachezaji wa ridhaa ambao ni division A,B,C, seniors,na ladies watacheza siku ya Jumamosi, Januari 29.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Lumuli Minga ambao ni wadhamini wa mashindano hayo, alisema ni jambo la furaha kwao kuendelea kutengeneza fursa mbalimbali.

“Katika hili shindano la Waitara Cup tupo kwa miaka mitatu na tutaendelea kuwa wadhamini, dhamira ni kuendeleza gofu nchini,” amesema Lumuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles