24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO 10 BORA KWENYE TAALUMA YA KILIMO, MISITU  

Na FARAJA MASINDE


 

Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Agrom ParisTech- UfaransaKILA taaluma duniani ina mahala pake, hali hii ndiyo inayosaidia kuwapo kwa vyuo vikuu mbalimbali ambavyo vimekuwa vikiongezeka kulingana na mabadiliko ya dunia.

Leo hii tunashuhudia kuendelea kushamiri kwa vyuo vinavyotoa taaluma ya gesi jambo ambalo ilikuwa si rahisi kwa miaka ya nyuma kuona vyuo vya namna hiyo.

Mara nyingi malengo ya kuanzishwa kwa chuo hususan hivi vya masomo maalumu huwa ni kutaka kuhakikisha kuwa vinatoa taaluma hiyo ipasavyo pasi na kuchanganya na masuala mengine ambayo yatasababisha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri na hivyo kushusha hadhi ya chuo.

Utaratibu huu wa kuanzisha vyuo maalumu kwa ajili ya taaluma husika ndio leo umesaidia mataifa mengi kujitengenezea majina makubwa katika utoaji wa elimu kwenye nyanja mbalimbali.

Yapo ambayo yamefanikiwa kujenga majina kupitia kubobea kwenye teknolojia, sheria, siasa, uchumi, elimu, mazingira, dini, sanaa na nyanja nyingine bila kusahau sekta ya gesi ambayo kwa siku za karibuni tumeaona taaluma hii ikianza kutolewa kwenye baadhi ya vyuo vikuu barani Afrika.

Kama hivyo ndivyo, basi leo ngoja tuangazie vyuo vikuu bora kwenye utoaji wa taaluma ya kilimo na misitu kwani ni eneo ambalo pia limekuwa likilalamikiwa kwenye maeneo mengi hususan nchi za Afrika ikiwamo Tanzania kuwa limekuwa likizorota kwa kukosa wataalamu.

Si kwamba hakuna vyuo vinavyotoa taaluma hii hapa nchini la hasha! vipo vingi tu kikiwamo Chuo Kikuu cha Kilimo mkoani Morogoro (SUA) na vinginevyo.

Hata hivyo, wengi wamekuwa wakiamini katika kusoma kwenye vyuo vikuu vya kimataifa kwa ajili ya kuwarahisishia kukuza wasifu wao ili hata wakienda kuomba kazi kwenye mataifa ya ng’ambo basi iwe ni rahisi kupata kazi kupitia vyuo hivyo.

Tayari shirika la utafiti wa vyuo vikuu duniani kwenye upande wa taaluma la QS World University Rankings, limevitaja vyuo vikuu ambavo ni bora kwenye utoaji wa taaluma hii ya kilimo na misitu ambapo unaweza kujipanga kwa ajili ya kwenda kubukua kuanzia mwaka huu.

Utafiti huu ulihusisha masomo 42 ambapo katika masomo hayo chuo kilikuwa kikitazamwa kwa vitu vingi ikiwamo namna ambavyo wanafunzi wake wamefanikiwa kuajiriwa kirahisi dunani kote, pia eneo la ufanyaji tafiti ambalo limekuwa likiangaliwa zaidi na mashirika mengi ya tafiti.

Eneo jingine lililozingatiwa mpaka kuhakikisha chuo kinapata nafasi ya kufuzu kwenye orodha hii ya vyuo bora kwenye utoaji wa taaluma hii ni pamoja na namna ambavyo wahitimu wake hata mara baada ya kuajiriwa utendaji kazi wao umekuwa ni wa namna gani.

Hapa tunazitazama kumi bora ya vyuo hivi ambavyo vimeweza kuongoza kundi hili la vyuo takribani 100 kwenye utoaji wa taaluma hii ambapo hata hivyo bado Marekani imeonekana kuwa kinara kwenye orodha hii ya 10 bora na alama zake kwenye mabano.

Chuo kilichoshika nafasi ya kwanza ni, cha nchini (96.10) cha Uholanzi kikifuatiwa na vyuo vikuu vya California Davis (94.70), California Berkeley (UCB(94.40) vyote hivi vikiwa ni kutoka nchini Marekani.

Vingine katika nafasi ya nne ni Agrom ParisTech (94.00) cha nchini Ufaransa, Chuo Kikuu cha Wisconsin Madision(85.00) cha Marekani, Swedish University of Agriculturtal Sciences(83.11) nchini Sweeden.

Vyuo vikuu vingine vinavyokamilisha kumi bora ni pamoja na kile cha Michigan State (81.00), Purdue University (82.80) huku nafasi ya kumi ikichukuliwa na chuo kikuu cha Iowa Satate(81.00) vyote hivi ikiwa ni kutoka nchini Marekani.

Hivyo, hapa uamuzi unabaki kwako kuangalia ni chuo gani unataka kwenda kusoma kati ya hivyo kumi ambavyo ni kinara kwenye utoaji wa taaluma ya kilimo na misitu.

Kwa faida yako tu chukua hii kuwa asilimia 61 ya wanafunzi waliohitimu kwenye vyuo hivi wamefanikiwa kuajiriwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles