22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

HANSPOPE: ANGBAN HAIDAI CHOCHOTE SIMBA

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM


Vicent AngbanUONGOZI wa klabu ya Simba umesema tayari umemalizana na aliyekuwa kipa wao, Vicent Angban raia wa Ivory Coast ambaye alikubali kuvunja mkataba wake katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo lililofungwa Desemba 15, mwaka jana.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa Kamati ya usajli ya klabu hiyo, Zacharia Hanspope, alisema kipa huyo hana anachoidai Simba kwani tayari ameshalipwa kulingana na makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kuvunja mkataba wake.

“Tulifanya makubaliano na kiasi tulichokubaliana alilipwa, hayo malipo ya miezi mitano yalikuwa ni madai yake kabla hatujafikia makubaliano, lakini baada ya kufikia mwafaka alilipwa na kuondoka nchini,” alisema.

Hata hivyo, Hanspope hakutaka kuweka wazi kipa huyo alibakiza mkataba wa muda gani na kiasi walichomlipa kama fidia ya kuvunja mkataba wake kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na pande zote.

“Hiyo ni siri ila tumemalizana vizuri na akaondoka kwa amani kwa sababu Simba hatuna tabia ya kumdhulumu mchezaji,” alisema Hanspope.

Kipa huyo aliyewahi kufanya majaribio katika klabu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza, alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili na kuitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja na nusu kabla ya kuondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kipa Mghana, Daniel Agyei.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles