Umsota kuongeza wanachama

0
628

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Umoja wa Wachezaji soka wa zamani Tanzania (UMSOTA) una mpango wa kuhamasisha wachezaji wa zamani kujiunga kwenye umoja huo.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Mwenyekiti wa UMSOTA,nFaza Lusozi, amesema tayari wameunda timu ya uhamasishaji ambayo itashirikisha magwiji wa mpira.

Amesema sasa wapo kwenye mchakato waliopata viwanja vya kufanyika mazoezi ili kuanza jukumu la uhamasishaji ambalo litaanza Dar Es Salaam na kufuatiwa mikoa mingine .

Mwenyekiti huyo amesema kuwa mpango huo itafanyika kwa mzunguko ili kuongeza idadi kubwa ya wanachama.

“Maandalizi yameanza kwa kuunda timu ya uhamasishaji ambayo itakuwa na jukumu la kuhamasisha watu wajiunge katika chama chetu,” amesema Lusozi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here