23.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Udalali ya Cityland yauza nyumba ya Ahsante Tour kwa milioni 600

Na Upendo Mosha, Moshi

Nyumba inayomilikiwa na kampuni ya utalii ya Ahsante Tous & Safaris Ltd ya mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro imepigwa mnada na kuuzwa kwa thamani ya Sh milion 600, baada ya kushindwa kulipa mkopo wa benki ya CRDB.

Nyumba hiyo iliyopo katika kata ya Kilimanjaro, Manispaa ya Moshi, mtaa wa Mawenzi, imeuzwa na Kampuni ya udalali ya jijini Arusha ya Cityland.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Cityland, John Muna, amesema taratibu zote za kisheria zimefuatwa katika uuzwaji wa nyumba hiyo,baada ya kapuni hiyo kushindwa kulipa deni lake.

Amesema mteja aliyebahatika kununua nyumba hiyo amekwisha weka kiasi cha fedha zilizohitajika kulingana na taratibu za mnada.

“Leo tumefanya mnada wa kuuza nyumba hii baada ya mmiliki wake kushindwa kulipa,tumepewa ridhaa hii na benk ya CRDB, taratibu zote tumezifuata na mteja amepatikana na ameinunu kwa Sh milion 600 kwa ajili ya kulipia deni lake,”amesema.

Upande wake mmliki wa kampuni ya, Ahsante Tous & Safaris Ltd, ambaye pia anamiliki hoteli ya kitalii, Cathibert Swai, amesema hawezi kuzungumzia lolote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles