Walimu wapigia hesabu pointi za ABC

0
571

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Kocha wa timu ya Walimu, Maka Mwalwisi ,amesema wanajipanga kupata matokeo mazuri na pointi tatu katika mchezo wa kesho.

walimu watatupa karata yao dhidi ya ABC katika mchezo wa Ligi Daraja la Nne utakaochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kigamboni.

Akimzungumza na www.mtanzania.co.tz, Maka ,amesema wachezaji wapo tayari na wamejipanga kufanya vizuri ili kutimiza malengo yao.

Amesema tayari amezifanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika mchezo uliopita na sasa kikosi kipo tayari kwa mapambano dhidi ya wapinzani wao.

“Mahitaji yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo wa Jumamosi tupate matokeo mazuri na tuvune pointi tatu ,” amesema Mwalwisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here