25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Tetesi za soka Ulaya

Lampard anukia Palace

ALIYEKUWA koha wa Chelsea, Frank Lampard, ameingia kwenye orodha ya makocha wanaofukuziwa na Crystal Palace.

Kocha Roy Hodgson ataondoka Palace baada ya kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na huenda ‘akasepa’.

Barca wateta na Flick

IMEFICHUKA kuwa Barcelona wameanza kuwasiliana na kocha aliyeachana na Bayern Munich, Hansi Flick.

Hiyo inamaanisha kuwa Barca watamfungulia mlango wa kutokea kocha wao wa sasa, Ronald Koeman.

United wamsogelea Romero

KLABU ya Manchester United inavutiwa na mpango wa kumsajili beki wa Kiargentina, Cristian Romero.

Mbali ya nyota huyo wa Atalanta, pia Man United inawataka Sven Botman (Lille) na Jules Kounde (Sevilla).

Howe aibukia Celtic

ALIYEKUWA kocha wa Bournemouth, Eddie Howe, amekubali kibarua cha kuinoa Celtic ya Ligi Kuu ya Scotland.

Howe amekuwa nje ya kazi ya ukocha tangu alipotemana na Bournemouth mwishoni mwa msimu uliopita.

Kocha mpya Spurs wiki ijayo

SIKU chache zijazo, mabosi wa Tottenham wataanza kufanya usahili wa kumsaka kocha mpya.

Hadi sasa, jina la kocha wa Fulham, Scott Parker, linatajwa zaidi, hasa baada ya Brendan Rodgers wa Leicester City kukataa.

Anayekiwa Arsenal aibuka

MSHAMBULIAJI wa Slavia Prague anayefukuziwa na Arsenal, Abdallah Sima, amesema anatamani kukipiga Ligi Kuu ya England.

Hiyo inakwenda kuwa habari njema kwa Washika Bunduki, sambamba na West Ham ambayo pia inamtrolea macho nyota huyo mwenye umri wa miaka 19.

Liver msikieni Klopp

MKUU wa benchi la ufundi la Liverpool, Jurgen Klopp, amesema hatarajii kufanya usajili ‘bab kubwa’ mwishoni mwa msimu huu.

Wakati huo huo, mchambuzi wa soka, Ian Wright, amemtaka kiungo wa Brighton, Yves Bissouma, kuikataa Liverpool ili ajiunge na Manchester United.

Arteta ataka wapya watano

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, ameagiza ashushiwe silaha tano za maangamizi kupitia dirisha kubwa la usajili wa kiangazi, mwaka huu.

Katika orodha yake, Arteta anataka mabeki wa pembeni wawili, kiungio wa ulinzi, straika na mlinda mlango.

Barca wammezea mate Buffon

KLABU ya Barcelona imeanza harakati za kumsaka mlinda mlango mkongwe wa Juventus, Gianluigi Buffon.

Buffon (43), amesahaweka wazi kuwa atatimka Serie A mwishoni mwa msimu, hivyo Barca washindwe wao tu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles