Mke wa Mugabe kufikishwa Mahakama ya Kitamaduni

0
527
epa04518454 A picture dated 06 December 2014 shows Zimbabwean first lady Grace Mugabe following proceedings during the last day of the Zanu PF 6th people's congress in Harare, Zimbabwe. Zimbabwean President Robert Mugabe was confirmed on 06 December as the leader of the ruling Zanu-PF party while his wife was also given a high-level position, boosting her chances of succeeding her husband. Grace Mugabe was endorsed as the head of the powerful Zanu-PF Women's League at a party congress. The 49-year-old has emerged as a possible successor to her 90-year-old husband, sidelining popular Vice President Joice Mujuru, whom Robert Mugabe has accused of plotting to assassinate him. In addressing the gathering Mugabe attacked the British government and that Zimbabwe will never be a colony again. EPA/AARON UFUMELI

-Harare, Zimbabwe

Mahakama ya Kitamaduni nchini Zimbabwe yamtaka Mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe kufika mahakamani hapo kwa tuhuma za kufanya mazishi “yasiyofaa” ya hayati Rais Robert Mugabe.

Grace Mugabe anatuhumiwa kwa kuenda kinyume na utamaduni wa jamii yao kwa kumzika mume wake katika boma la familia badala ya kumzika sehemu iliyochaguliwa na jamaa zake na mama yake.

Katika waraka kutoka kwa Chifu Zvimba, ambaye ni mkuu wa kitamaduni wa nyumbani kwa kina Mugabe amesema Grace anatakiwa kuufukua mwili wa hayati Rais Mugabe ili uzikwe tena kulingana na utamaduni wa watu wa Zvimba.

Pia ameagizwa kulipa faini ya ng’ombe na mbuzi kwa kukiuka utamaduni.

Mugabe alifariki mwaka 2019 katika hospitali moja nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95.

Familia yake iliamua afanyiwe mazishi ya faragha kijijini kwao Kutama wilaya ya Zvimba- karibu kilomita 90 sawa na (maili 55) magharibi mwa mji mkuu wa Harare, baada ya mvutano wa wiki kadhaa na serikali.

Patrick Zhuwao, mpwa wa marehemu rais alisema kwamba Mugabe alizikwa kulingana na ombi lake, uamuzi ambao unastahili kuheshimiwa.

Pia hakuna mzozo ndani ya familia akiongeza kwamba suala hilo lipo nje ya mamlaka ya chifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here