26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Takukuru: Tumeokoa Sh bilioni 70

Na SARAH MOSES,-DODOMA.

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Othumani, amesema oparesheni zilizotekelezwa na chombo hicho  zimeokoa Sh bilioni 70.3.

Hayo aliyasema   Dodoma jana wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Takukuru  uliokuwa ukieleza utendaji kazi kwa kipindi cha  Julai mwaka 2017 hadi Juni 2018.

Alisema taasisi hiyo iliweka mkazo katika maeneo yaliyo lalamikiwa zaidi yale yenye athari katika uchumi kama ubadhirifu wa fedha za umma zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Vilevile tu lijikita kwenye matumizi mabaya ya madaraka na ukwepaji kodi na maduhuli ya serikali,” alisema Othumani.

Pia alisema idadi ya kesi zilizofunguliwa mahakamani zimeongezeka, ikiwamo kiwango cha kushinda kesi na kiwango cha fedha kilichookolewa kwenye oparesheni pia kimeongezeka.

“Majalada 906 yalichunguzwa na kukamilika, vilevile kesi 495 zilifunguliwa mahakamani,” alisema.

Wakati huohuo, alisema katika kipindi hicho, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchi nzima ulifanyika   kuhakikisha thamani ya fedha inapatikana katika kila mradi.

“Takukuru ilifuatilia miradi 661 ikiwamo ile mikubwa minane ya maji yenye sura ya  taifa na ilikuwa na thamani ya takribani Sh bilioni45.

“Ufuatiliaji huu ulibaini vitendo vya rushwa na ubadhirifu,  pia hatua kadhaa zimeshachukuliwa kukabilianana matatizo yaliyobainika,” alisema.

Pia alisema  tangu ateuliwe zaidi ya kesi 65 zimefikishwa mahakamani.

Alisema mojaya changamoto wanayokabiliwa nayo ni uchakavu wa vitendea kazi yakiwamo magari,vifaa vya  uchunguzi na thamani za ofisini.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika alisema   Takukuru itafanikiwa na mapambano dhidi ya rushwa iwapo wananchi watakuwa na imani nao.

“Wananchi wakijua kama nyinyi mnatoa taarifa mnazopelekewa kutoka 113, wakijua taarifa mnazo pata mnawapelekea watuhumiwa wenyewe halafu mkaenda kuwadai rushwa, taarifa hizo hamtazipata tena.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,277FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles