26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Miaka 50 ya Bakwata itumike kujitathmini

MNa CLARA MATIMO

DESEMBA 17, mwaka huu Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), linatarajia kufanya maadhimisho ya kutimiza miaka 50 tangukuanzishwa kwake.

Maadhimisho hayo ya kitaifa ambayo yanatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam, ni ya kwanza tangu baraza hilo lilipoanzishwa Desemba17, 1968 mkoani Iringa.

Bakwata lilianzishwa kwa lengo la kuwaunganisha Waislamu wapate chombo cha kuwasemea, kuendeleza elimu kwa Waislamu, kutoa malezi namaadili mema kwa vijana, kuratibu shughuli zote za taasisi za Kiislamu nchini,kulinda na kusimamia mali za baraza hilo.

Tangu lilipoanzishwa baraza hilo limeongozwa kwaawamu tatu, ambapo Sheikh Hemed Jumaa aliongoza kwa mara ya kwanza hadi mwaka2002, akafuatiwa na Issa Simba aliyedumu hadi mwaka 2015 na Sheikh Abubakar Zubeir aliyepo kwa sasa.

Naamini kila uongozi uliopita unayo mambo mazuri uliyoyafanya kwa masilahi ya Waislamu wote nchini hususan awamu ya sasa chini ya Mufti Sheikh Zubeir ambaye tangu aingie madarakani amejipambanua kwa kauli mbiu ya ‘Jitambue, Badilika acha Mazoea’.

Kauli mbiu hiyo imelenga kuleta mageuzi makubw andani ya baraza hilo kwa kuhimiza kila Mwislamu kuishi katika misingi mizuri yadini na viongozi wa Bakwata kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kurejeshaimani iliyokuwa imeanza kutoweka.

Kutokana na baadhi ya viongozi wa baraza hilo kutokanje ya mstari, kulizua maswali kwa waumini walioanza kuitupia lawama Bakwata kwa kushindwa kutoa malezi na maadili mema kwa vijana, kuratibu shughuli zote za taasisi za Kiislamu nchini, kulinda na kusimamia mali zabaraza hilo.

Hali hii pia ilithibitishwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Bakwata Mkoa wa Mwanza, Rajabu Rajabu, ambaye anaaminikuwa Bakwata ililala na kushindwa kusimamia majukumu yake ikiwemo malezi, hivyokutoa mwanya kwa baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema kuwapa mafundisho mabayana kusababisha baadhi ya vijana kujihusisha na masuala ya ugaidi.

Hivyo basi kutokana na udhaifu huo nakubaliana na hoja ya Katibu wa Msikiti wa Ijumaa uliopo jijini Mwanza, Abdallah Sheikh Amin, aliyeitaka Bakwata kuangalia namna bora ya kupata viongozi wake na kuepuka kuwapa nafasi ya kutoa elimu katika misikiti masheikh na maimamu ambao hawajulikani.

Hii itasaidia vijana kutopata mafundisho ambayo hayaendani na maadili ya dini ya Kiislamu maana kijana wa Kiislamu kujihusishana vitendo vya ugaidi ni kuutukanisha Uislamu kwa kuwa mafundisho ya dini hiyo haya ruhusu muumini yeyote kutenda mambo mabaya katika jamii. 

Rai yangu kwa viongozi na Waislamu wote nchini wahakikishe wanatumia maadhimisho haya ya miaka 50 ya Bakwata kwa ajili yakujitathmini kwa kuyafanyia marekebisho na kuondoa kasoro zinazoleta msuguanona kusababisha kushindwa kutimiza matakwa ya waumini wa dini hiyo pamoja nakuratibu shughuli zote za taasisi za Kiislamu nchini.

Kama ambavyo tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa Bakwata wakisimamishwa uongozi kwa madai mbalimbali ikiwemo kushindwa kusimamia vyema mali za baraza hilo zilizopo katika mikoa yao jambo lililosababisha maliza Waislamu kuhujumiwa.

Katika kuhakikisha baraza hilo linarudi kwenye misingi yake na malengo mahususi, Mufti Abubakar Zubeir, aliunda tume kufuatilia mikataba yote ya uuzaji wa viwanja na mali za baraza na taasisi zake nchi zima na kuona uhalali wa umiliki huo pamoja na hali ya usajili wa mali hizo.

Pia katiba ya Bakwata imefanyiwa marekebisho katika kipengele cha uongozi na sasa masheikh wa mikoa na wilaya watapatikana kwa kuteuliwa na wajumbe wa baraza la ulamaa la Bakwata taifa.

Mabadiliko haya ya Katiba yamewafurahisha Waislamu wengi akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu Bakwata Mkoa wa Mwanza, Mohamed Ngonyoke, anayeamini kwamba mfumo huo utaleta ufanisi ndani ya Bakwata kwa kuwa viongozi hao wanaelewa wasipowajibika uteuzi wao utatenguliwa tofauti na ule waawali uliokuwa unawalinda hadi kifo.

Ni wazi kwamba tangu kufanyika mabadiliko haya mpaka sasa mikoa yote haina masheikh wakuu bali wapo makaimu ambao wanasubiria uteuzi.

Ni imani yangu kuwa wale watakaopata nafasi za uongozi watawajibika ipasavyo kwa masilahi ya Waislamu na miaka hii 50 iwe sehemu ya wao kujitathmini na kujifunza.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,277FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles