24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SSRA yakoromea Mifuko  Hifadhi kuishi kwa kipato  

irene-kisakaNa Mwandishi Wetu

Suala la mifuko ya jamii ni muhimu katika uchumi wa kileo na Tanzania kama nchi inazingatia uweko wa mifuko hiyo na imeunda Mamlaka ya Mifuko ya Jamii  (SSRA) ili kuisimamia mifuko hiyo kwa kuiendesha kwa ufanisi unaotakikana.

Wajibu wa SSRA kuundwa kwake mwaka 2008 kutokana na  kifungu cha 5(i) cha sheria  ya Mamlaka ni Usimamizi wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii ni pamoja na kusajili mifuko, Watunzaji na Meneja wa Uwekezaji  katika sekta ya Hifadhi ya Jamiii, kudhibiti,  kurekebisha na kusimamia  utendaji wa mifuko, watunzaji na mameneja wa Uwekezaji na kutoa miongozo kwa ajili  ya usimamizi  na uendeshaji  wa sekta ya hifadhi ya jamii na kutetea kwa kulinda  maslahi ya wanachama.

Kazi nyingine ni kusajili na kusimamia  wasimamizi  katika sekta  ya hifadhi ya Jamii  na kumshauri Waziri juu ya Sera  na masuala ya kiutendaji  yanayohusiana  na Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Masuala mengine ni kutoa muongozo  kwa mifuko , watunzaji  kumbukumbu na Mameneja  wawekezaji.

SSRA inasimamia mageuzi ya Sekta ya Hifadhi ya Janii kwa kuanzisha mafunzo, kushauri, kuratibu  na kutekeleza  mabadiliko  ya sheria  katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii na vilevile kumteua msimamizi wa Mifuko pale inapobidi .

Lakini  SSRA inatakiwa kurahisisha  upanuzi wa wigo wa Hifadhi ya Jamii kuwafikia wale  ambao bado hawajafikiwa ikiwa ni  pamoja na  makundi/ sekta zisizo rasmi na kuendesha mipango ya elimu   na uhamasishaji  kwa umma  juu ya masuala  ya hifadhi ya Jamii.

“Kwa kutekeleza masuala hayo  nyeti  inahitaji mipango thabiti na kuzingatia mwenendo usiotiliwa shaka na hivyo kuwa  na uadilifu, utendaji kazi wa pamoja , ubunifu na usiri kwa kuhakikisha kuwa na siri kwq wadau wake  kwa taarifa na maoni  yoyote ya binafsi  kwenye masuala nyeti  yanabaki kuwa siri, “ anasema Irene Kisaka Mkurugenzi Mkuu wa SSRA.

SSRA  inatakiwa kuwa na weledi  kwa kufanya na kuwatumia wataalamu  waliobobea kwa kuweka miongozo mahiri itakayowezesha kulinda  maslahi ya  wanachama  na utoaji  huduma  bora za Hifadhi ya Jamii  na hivyo kutoa huduma  zinazolenga  mteja  kwa kuwatambua  kote waliko ja kuwafuata kutoa huduma stahiki..

Ikiwa na mwongozo ulioelezwa hapa kwa mapana SSRA imeanza kuona mmomonyoko wa madili kwenye mifuko baada ya kubaini kuwa baadhi ya mifuko imeanza kuwa  na mapungufu kwa kuishi bila kuzingatia  sheria ambayo kwa siku za karibuni  kunaonesha gharama za uendeshaji na utawala kuzidi kiwango kilichoruhusuiwa  cha asilimia 10 ya makusanyo ya mfuko husika na hivyo kuwa kinyume na taratibu.

SSRA  imetoa mwongozo  kuhusu suala la hilo na kutaka mifuko kurekebisha hali hiyo ndani ya miaka miwili  ijayo ili mambo yaende sawa na wale  ambao matumizi yao ni chini ya kiasi hicho na wanotaka kuongeza matumizi yao wtafanya hivyo kwa kuzingatia matumizi yasizidi  kiasi cha asilimia 0.1 ya kipatochake cha makusanyo kwa mwaka.

Mamlaka inaweza kuondoa kikwazo hicho kwa kuzingatia mahitaji halisi ya mfuko au mifuko ili kuongeza ukuaji wa mfuko na kuongeza tija  kwa maslahi makubwa ya wanachama  na skimu hiyo kwa muda  utakaopangwa na sio vinginevyo.

Mkurugenzi wa SSRA  wa masuala ya Sheria, Ornorius Njole amesema mwaka huu mwezi Julai kuwa mwongozo wa kuendesha mifuko umetolewa na umeanza kutumika kufuatia kuzidi kwa uvunjaji wa taratibu  kwa baadhi ya mifuko kuhusu matumizi.

Njole  alisema hayo wakati wa mkutano na Wahariri  jijini akiwafahamisha maendeleo mbalimbali ya Mamlaka na kutoa maelezo muafaka juu ya kutokuwepo kwa fao la kujitoa katika huduma za mifuko ya jamii jambo tete kwa baadhi ya wanachama haswa wa migodini.

Amesema badala ya fao la kujitoa kuna fao la kukosa ajira na linatakiwa  kuziba pengo la watu kukosa kipato na akasema mafao yataanza kutumika karibuni na huku utafiti utafanyika kwa kina kujua kwa nini  mifuko0 inazidisha matumizi kinyume na taratibu.

Alitanabahisha kuwa fao la kukosa  au kupoteza ajira  litatolewa kwa miezi sita ikiwa asilimia 33 ya mshahara wa mwisho wa muathirika na hivyo kupunguza makali ya maisha.

Mwongozo huo uko bayana kwa wale wanaovunja taratibu kwa kutoa adhabu au mwongozo kimaandishi namna ya kurekebisha kasoro  au kuonesha nia ya kuiadhibu Bodi ya Wadhamini ya Skimu  na Utawala na kutoa mapendekezo kwa mamlaka za uteuzi kwa hatua au kuchukua hatua yoyote inayoonekana kuntu kwa hali yenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles