23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania ya kumi uwekezaji, ya  pili kukua uchumi Afrika

tpsfNa Joseph Lino

Tanzania inashika nafasi ya 10 katika uwekezaji wa nje barani Afrika baada ya kuongezwa kwa miradi mikubwa 20 mwaka jana.

Ripoti ya Uwekezaji  Kutoka Nje (FDI) bara la Afrika iliyotolewa na Financial Times kutoka nchini Uingereza wiki iliyopita inaangalia maendeleo ya uchumi kwenye makampuni makubwa yaliyowekeza Afrika kutokana na mitaji ya miradi mbalimbali.

Kwa maelezo ya ripoti hiyo, inaonesha  nchi 10 zilizoongoza katika uwekezaji wa nje kwenye miradi mwaka 2015 Tanzania na Uganda wamefungana kwenye nafasi ya kumi.

Nchi hizi mbili za Jumuia ya Afrika Mashariki zote  zilifanikiwa kupata miradi ya uwekezaji wa nje 20 kila moja, wakati  Kenya inashika nafasi ya pili ikiwa na miradi 85.

Orodha kamili inaonesha kuwa Afrika Kusini iliongoza  kwa miradi 118, Kenya (85) Misri 59, Nigeria 51, Ghana 40, Msumbiji 29, Ethiopia 27, na Cote d’Ivoire 26.

Mhariri wa ripoti hiyo, Adrienne Klasa anasema kuwa “ikiwa nchi zenye uchumi mkubwa zinayumba kiuchumi, baadhi ya nchi  ndogo katika uchumi zinaendelea kufanya vizuri kama Tanzania, Senegal na Cote d’Ivoire kwa uchumi wao unakua kwa kasi,”

Nchi 10 za Afrika zilizoongoza katika mitaji mikubwa ya uwekezaji  kutoka nje, ni Misri dola za kimarekani bilioni 14.5, Nigeria, bil 8.6, Msumbiji bil.5.1, Afrika Kusini, bilioni 4.7, Morocco, 4.5, Cote d’Ivoire 3.5, Angola 2.7, Kenya 2.4, Senegal 1.9 na Cameroon bilioni 1.8.

Ripoti hiyo inaelezea kuwa nchi za Ulaya zinaongoza katika mitaji ya uwekezaji kufikia dola bilioni 30.1 kwa  mwaka jana.

Italy iliwekeza miradi  ya thamani ya dola bilioni  7.4, hata hivyo China inashika nafasi ya 9 kwenye mitaji ya uwekezaji na nafasi ya 7 katika kuwa na miradi mingi ambayo iliweza kutengeneza ajira 14,127 barani Afrika kote mwaka jana.

Jumla ya makampuni 495 yaliwekeza mwaka jana ukilinganisha na makampuni 469 mwaka 2014.

Maeneo yaliyoongoza kwenye uwekezaji ni huduma za biashara, mauzo na masoko na sekta ya viwanda.

Sekta ya fedha iliongoza kwa kuwa na idadi nyingi ya miradi ambayo ilifikia 118 kwa mujibu wa ripoti.

Sekta ya mafuta na gesi ilishika nafasi ya juu kwa mitaji mikubwa ya uwekezaji iliyofikia dola bilioni 15.7

Nchi ambazo zinatarajia uchumi wake kukua kwa kasi mwaka huu  ni Cote d’Ivoire uchumi wake unategemea kukua kwa asilimia 8 huku Tanzania ikishika nafasi ya pili kwa asilimia 7.

Marekani ilikuwa moja wa wekezaji wakubwa Afrika hata hivyo imeshuka kwa asilimia 4 katika idadi ya miradi, ambayo thamani yake ilishuka kwa asilimia 12 ambayo ni sawa na dola bilioni 6.8

Pia Uingereza ilishika nafasi ya pili ikiwa  na idadi ya miradi kuongezeka kwa asilimia 50,  miradi ya uwekezaji ilifikia 76, ambapo mitaji ya uwekezaji ya nje iliongezeka kwa asilimia 93.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles