31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Rani yaanza kufanya kweli Ligi Kuu Wanawake

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

MDHAMINI mwenza wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, Rani Sanitary Pads ambao ni wauzaji wa taulo za kike, wameanza kufanya kweli kuhakikisha ligi hiyo inazidi kuwa na ushindani baada kutoa tuzo kwa mshambuliaji wa Simba Queen, Oppa Clement na kiasi cha fedha sh. 500,000.

Oppa ambaye kwa sasa ndiye kinara wa mabao akifikisha 19 katika mechi 11 alizocheza, anakuwa mchezaji wa kwanza wa ligi hiyo kupata tuzo hiyo itakayokuwa inatolewa kila mwezi na wadhamini hao.

Rani ilimkabidhi Oppa tuzo hiyo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wa Simba Queens dhidi ya Fountain Gate ya Dodoma iliopigwa kwenye Uwanja wa MO Simba, Dar es Salaam ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Ofisa Masoko wa Rani Sanitary Pads, Raphia Yusuf akimkabidhi tuzo mchezaji wa Simba Queens Oppa Clements.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Oppa amesema hali hiyo inaongeza hamasa na ushindani kwa wachezaji ambapo kila mmoja atatamani kuibuka mshindi.

“Binafsi nimependa hiki kitu maana kitaongeza hamasa ya kupambana ndani ya ligi yetu. Nawashukuru wadhamini kwa kutambua mchango wetu na kutuandalia tuzo kama hivi,” amesema Oppa.

Kwa upande wake Mratibu wa Rani Sanitary Pads, Abdulah Mkeyenge, amesema wameamua kutoa tuzo hizo ili kuliheshimisha soka la wanawake na anaamini wao wanakuwa wadhamini wa kwanza kutoa tuzo kama hiyo.

“Sidhani kama iliwahi kutoa kiti kama hiki tulichofanya cha kutoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi ya wanawake, mara nyingi nafanyika kwa wanaume.

Aidha katika hatua nyingine wametoa zawadi ya taulo za kike kwa kikosi cha Fountain Gate kama walivyofanya kwa timu nyingine.

Wachezaji wa timu ya Fountain Gate wakiwa wameshika taulo za kike walipoewa zawadi ya Rani Sanitary Pads

Mtendaji Mkuu wa Rani Sanitary Pads, Ramadhan Badi, amesema amefurahi kumalizana na Fountain Gate ambao ndiyo timu pekee iliyokuwa imebaki.

“Ligi yetu ina timu 12, tumeshatoa taulo hizo kwa timu 11 z kama zawadi, waliokuwa wamebaki ni hawa Fountain Gate, tunashukuru kumalizana na zoezi hili na kinachofuata ni utoaji wa elimu kwa wachezaji wa timu zote,” ameeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles