28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Peaktime Media kuibua vipaji vya masumbwi mtaani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya inayojihusisha na michezo ikiwamo masumbwi nchini, Peaktime Media imesema imedhamiria kuibua vipaji vya mchezo wa ngumi kwa kufanya mashindano katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Peaktime Media ilizindua tamasha la kumtafuta bondia nyota wa Mtaa ililopewa jina la ‘Champion wa Kitaa’, Tandika jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ujio wa tamasha hilo, Mratibu Mkuu wa Peaktime Media, Meja Seleman Semunyu, amesema lengo ni kuibua na kuendeleza vipaji vya ngumi ambavyo havipewi kipaumbele katika mchezo huo.

“Baada ya mapambano haya, kutakuwa na mapambano makubwa kati ya Wilaya na Wilaya katika mkoa wa Dar es Salaama na mwaka huu kabla haujaisha naamini kutakuwa na pambano kubwa zaidi,” ameeleza Meja Semunyu.

Amesema baada ya Tandika, kituo kinachofuata kumsaka Champion wa Kitaa kitakuwa ni Mbagala Februari 20, 2022 kwenye Ukumbi wa Dar Live.

Aidha mabondia wakongwe wa uzito wa juu, Alphonce Mchumiatumbo na Alex Sitampini wanatarajia kupanda ulingoni kuonyeshana kazi mwaka huu katika pambano la uzito wa kilo 91.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles