23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DC Irando ataka ubora wa miradi ya barabara

Na Omary Mlekwa, Hai

MKUU wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Juma Irando amewataka Wakandarasi waliopata kazi za wakala wa barabara za Vijiji na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanazingatia mikataba yao na kusisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuona mikataba inapita muda wake wa utekelezaji na kutekeleza miradi hiyo kwa viwango na ufanisi unaotakiwa ili kuendana na thamani ya fedha.

MKUU wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Juma Irando akisisitiza jambo kwa
Meneja wa TARURA wilayani hapa, Mhandisi Rckson Lema, baada ya kukagua miradi ya matengenezo ya barabara.

Irando alitoa angalizo hilo wakati akikagua miradi ya matengenezo ya barabara inayotekelezwa (TARURA).

Irando amesema serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji barabara, hivyo ni lazima wakandarasi kufuata mikataba yao kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha.

“Sote tunafahamu umuhimu wa Sekta ya Barabara ni kiungo muhimu cha uchumi wa wananchi wetu. TARURA Mmepewa sekta nyeti ya kuchangia uchumi katika nchi yetu, tunahitaji kuona kasi.

“Katika maeneo machache ambayo hayafanyi vizuri tuongeze nguvu ya kusimamia kwa ukaribu zaidi ili wananchi waliotupa dhamana hii waweze kuona malengo ya uanzishwaji wa TARURA yanaendana na dhamira ya rais wetu,” amesema Irando.

Hata hivy, mkuu huyo wa Wilaya amemtaka Meneja wa TARURA wilayani hapa, Mhandisi Rickson Lema kuhakikisha kila mradi wa Barabara unaosainiwa utekelezwe ndani ya kipindi cha mkataba, na kuongeza kuwa hatokubaliana na utaratibu wa kuongeza muda wa mikataba kwa Wakandarasi kama hakuna sababu za msingi.

Zaidi alisisitiza: “Kumekuwa na changamoto ya mikataba kutotekelezwa kwa wakati, mikataba inasainiwa lakini haimaliziki kwa wakati, hivyo tunalazimika kuongeza muda wa utekelezaji wake jambo ambalo linaongeza gharama, linapunguza thamani ya fedha na kupunguza ufanisi wa malengo ya Serikali, hivyo basi ni vyema mikataba yote ya ujenzi wa barabara ikazingatia masharti yaliyopo kwenye mikataba ili kuondoa changamoto hii,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Hai, Denis Muyinga amewataka wakandarasi hao kuhakikisha kuwa wanakamilisha miradi hiyo mapema kulingana na mikataba yao na kutokuwa na sababu kwa baadhi ya wakandarasi hutafuta sababu za hali ya hewa pindi wanaposhindwa kukamilishwa kwa wakati.

Nae Meneja wa TARURA Ricksoni Lema alisema Serikali kwa mwaka wa 2021 /2022 inatekeleza miradi nane ya matengenezo ya barabara yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2.5 zinatumika kutengeneza kwa kiwango cha Changarawe, kujenga makalavati pamoja na kujenga mifereji kwa maji yasiweze kuharibu miundo mbinu hiyo pindi mvua zinaponyesha

Amefafanua kuwa baadhi ya barabara kazi zinaendelea huku nyingine zikiwa zimekalika ambapo amesema kuwa Barabara ya Makoa Darajani hadi Mferejini yenye urefu km 18.25 amesema kazi inaendelea kwa kufyeka na kuondoa vichaka vilivyopo eneo la barabarani ilio kupata upana unatakiwa pamoja na kukata ngema na kutanua barabara eneo la mlima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles