30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

RAIS WA KOREA KUSINI AONDOKA RASMI IKULU

Seoul, Korea Kusini


RAIS wa Korea Kusini aliyetimuliwa madarakani, Park Geun-hye, ameondoka rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo mjini Seuol.

Park ameondoka Ikulu na kwenda  nyumbani kwake Kusini mwa Seoul, kwa mujibu wa msemaji wake Ikulu, Kim Dong-jo.

Alifukuzwa  baada ya Mahakama ya Katiba nchini humo kuafiki uamuzi wa kuondolewa kwake kwa   kashfa ya kupotea kwa mabilioni ya fedha wakati wa utawala wake.

 Park sasa amepoteza  uwezo wa kutofunguliwa mashtaka ambao marais huwa nao, na huenda akakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa fedha.

Serikali ya Korea ya Kaskazini imepongeza  kuondolewa kwake akiwa ni mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles