23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEINGIA IKULU MAREKANI KUFUNGWA MIAKA 10

WASHINGTON, Marekani


MWANAMUME mmoja aliyekuwa amebeba mkoba na kuingia Ikulu ya Marekani kwa  kuruka ukuta, alikamatwa juzi na maofisa wa usalama.

Kosa hilo  ni la kuhatarisha usalama wa nyumba ya rais wa Marekani.

Rais Donald Trump alikuwamo ndani wakati Jonathan Tran mwenye umri wa miaka 26 aliporuka ukuta wa saa 5:38 usiku.

Taarifa ya maofisa wa usalama ilisema Tran alikamatwa na wanasalama wenye nguo za raia.  Tran mkazi wa California anashikiliwa bila dhamana.  

Raisi Trump aliwashukuru maofisa wa usalama kwa kumtia mbaroni kijana huyo.

Kwa mujibu wa Msemaji wa ofisi ya Mwanasheria Kuu wa Marekani,   Bill Miller, Tran anashitakiwa kwa kuingia eneo ambalo mtu harusiwi akiwa amebeba silaha ya hatari, na anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles