23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP AMTIMUA MWENDESHA MASHTAKA  

Washington, Marekani


MWENDESHA mashtaka wa   Marekani, Preet Bharara (46) amefukuzwa kazi na Rais   Donald Trump.

Bharara aliteuliwa na Rais aliyetangulia, Barack Obama, alishauriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu kujiuzulu.

Mwendesha mashtaka huyo  alikataa kujiuzulu, baada ya kuambiwa binafsi na Trump, baada ya uchaguzi mkuu wa urais  Novemba mwaka jana.

Kupitia mtandao wa jamii wa Twitter, Bharara, ameandika kuwa hajajiuzulu bali amefukuzwa kazi.

"Kutumikia nchi yangu ya Marekani kama mwanasheria kwa miaka saba imekuwa heshima kubwa ya maisha yangu na  taaluma.

“Bila kujali nitafanya nini au muda gani nitaishi ," Bharara alisema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles