MOURINHO ETI AMEKUWA ‘MNYENYEKEVU’ GHAFLA

0
462

ADAM MKWEPUNA MITANDAO


KOCHA Jose Mourinho amefurahia ushindi wa Ligi ya Europa, akiuhita ushindi wa Wanyenyekevu wasioonge-ongea sana kama washairi, akisema ni taji lake la mwisho.

Kocha huyo wa timu ya Manchester United amekiri kwamba alijihisi ni kocha mbovu zaidi duniani katika kampeni za msimu uliopita, hadi pale ambapo Manchester United walitwaa taji la Ligi ya Europa na kufanikiwa kutinga Ligi ya Mabingwa mwakani.

Man United ya Mourinho sasa imerejea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Ajax 2-0 na kuondoka na ndoo ya Europa.

Baada ya kumaliza nafasi ya sita kwenye michuano ya Ligi Kuu Uingereza pamoja na majeraha ya Zlatan Ibrahimovic, Marcos Rojo na Luke Shaw, Mashetani Wekundu walielekeza macho yao kwenye fainali ya Kombe la Europa, ambako kiungo Paul Pogba na Henrikh Mkhitaryan walihakikisha msimu wa United unamalizika wakiwa na taji la tatu mkononi, baada ya kutwaa Ngao ya Jamii na Kombe la EFL.

Mourinho alisherehekea taji lake la nne Ulaya kutoka kwenye fainali nne, Mreno huyo amebainisha kuwa amekuwa akijitilia mashaka yeye binafsi.

 “Washairi ni wale wanaoshinda kila mechi, wanashinda kila mechi. Nadhani kazi inakuwa nzuri kama ukishinda kila mechi. Sijawahi kushinda kila mechi. Baadhi ya watu hushinda kila mara, lakini mimi siwezi, sishindi.

 “Lakini katika msimu mbaya, msimu ambao wakati mwingine nilihisi timu yangu ni mbaya, mbovu kuliko zote duniani na nilijihisi kuwa kocha mbovu kuliko wote duniani lakini tumefanikiwa kutwaa mataji matatu na tunakwenda kucheza Ligi ya Mabingwa kwa kutwaa taji, bila kumaliza nafasi ya tatu au ya nne,”anasema Mourinho.

Mouringo anasema ushindi wa United unatokana na nadharia ya vitendo, si ushairi, bali watu wanyenyekevu.

Mreno huyo  ambaye alimrithi Van Gaal akitokea Chelsea msimu wa 2015/16 aliendelea: “Kwangu mimi hili ni taji muhimu sana katika taaluma yangu kwa sababu ni la mwisho.

 “Ndio maana nina mtazamo huu. Kiukweli Ligi ya Mabingwa ni kubwa kuliko Ligi ya Europa lakini hili ndilo taji la mwisho na taji la mwisho ni lile ambalo hisia zipo chini ya ngozi, hisia za kipekee.

Man United wanatarajia kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani baada ya kuondoka na taji hilo muhimu na kuusafisha msimu wao uliokuwa na madoa mengi wakishindwa kutinga nne bora Ligi Kuu Uingereza.

Mabingwa hao wanatarajia kuweka kikomo cha kufanya usajili kwa wachezaji watatu au wanne muhimu katika dirisha kubwa la usajili hivi karibuni.

Mourinho anasema makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward anafahamu  wachezaji wanaotakiwa kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita.

"Ed Woodward anayolisti yangu ya wachezaji ninaowataka ," anasema kocha  huyo baada ya mchezo wa Europa ligi dhidi ya Ajax .

Mourinho anataka kuongeza changamoto katika safu ya ulinzi na ushambuliaji ili kuweza kuwania taji la ligi kuu ya England msimu ujao.

United wamekua wakihushwa na kutaka kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kuwasajili Antoine Griezmann toka Atletico Madrid, Andrea Belotti wa Torino pamoja Romelu Lukaku.

Kwa Upande wa safu ya ulinzi wachezaji wanaotajwa kuwa wako kwenye rada ya Mourinho ni beki wao wa zamani Michael Keane anayechezea Burnley, beki kisiki wa Benfica Victor Lindelof na Muholanzi Virgil van Dijk wa Southampton.

Kipa wa United,  David de Gea,ambaye alikuwa  benchi akimtazama Sergio Romero aliyepangwa  kwenye mchezo  wa fainali ya Ligi ya Ulaya  huenda akaachana na timu hiyo na kujiunga na Real Madrid hivyo Mourinho anatakiwa kuangalia mbadala wa kipa huyo.

Ubora wa Eric Bailly,  tangu anunuliwe akitokea  Villarreal kwa pauni milioni 30 unazidi kuongezeka pamoja na  Marcos Rojo lakini shaka iko juu ya uwezo wa Phil Jones na  Chris Smalling.

Wakati huo nahodha wa United akiwa mbioni kuachana na timu hiyo msimu huu baada ya kudaiwa kutaka kurejea Everton.

Hata hivyo mashaka zaidi yapo katika afya ya Zlatan Ibrahimovic kutokana na kusumbuliwa na maumivu yake ya kifundo cha mguu na kusababisha hofu  na hatima yake ndani ya klabu hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here