JAQUELINE WOLPER: KIINGEREZA KIKWAZO KWETU

0
1195

Na BRIGHITER MASAKI


MSANII wa filamu nchini, Jacqueline Wolper, ameweka wazi kwamba wasanii wengi wa Tanzania wanashindwa kufanya filamu na wasanii wa nje kwa sababu hawaifahamu vyema Lugha ya Kiingereza.

Wolper alisema kwake lugha ya kiingereza ni changamoto kubwa ndiyo maana hawezi kufanya filamu za kushirikiana na wasanii wa nje kama baadhi ya wasanii wanavyofanya.

“Wasanii wachache ndio wanaojitahidi kwenda kufanya kazi na wasanii wa nje, mimi na baadhi ya wasanii wengine hatuwezi kushirikiana na hao kwa kuwa hatujui Lugha ya Kiingereza kwa ufasaha kwa kuwa filamu nyingi huzungumzwa kiingereza,’’ alisema Wolper.

Aliongeza kwamba kwa sasa ana mwalimu kwa ajili ya kuboresha kiingereza chake ili atimize ndoto zake za kucheza filamu na wasanii wa nje kwa lugha ya kiingereza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here