22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

Mke wa Waziri Mkuu Malaysia ashtakiwa

KUALA LUMPUR, MALAYSIA

MKE wa Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Najib Razak ameshtakiwa kwa makosa 17, ikiwemo utakatishaji wa fedha.

Hilo limekuja wakati, ambao maafisa wa kupambana na rushwa wakichunguza upotevu wa mabilioni ya dola kutoka hazina ya serikali.

Mashtaka dhidi ya Rosmah Mansor yalisomwa juzi na waendesha mashtaka katika Mahakama ya Kuala Lumpur.

Rosmah alikamatwa siku ya Jumanne na maafisa wa Tume ya Kupambana na Rushwa (MACC) na alilala mahabusu.

Hata hivyo, amekanusha mashtaka hayo huku mumewe Najib akikabiliwa na makosa 32 kuanzia utakatishaji fedha hadi matumizi mabaya ya madaraka.

Naye amekanusha tuhuma hizo dhidi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles