32.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza yaishutumu Urusi kwa mashambulizi ya kimtandao

LONDON, UINGEREZA

UINGEREZA imeishutumu Idara ya Ujasusi ya Kijeshi ya Urusi (GRU) kwa kuendesha mashambulizi kadhaa ya kimtandao ili kuhujumu demokrasia ya nchi za magharibi.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo chake cha Taifa cha Usalama Mitandaoni (NCSC), GRU  ilitumia mtandao wa wadukuzi kusambaza  taarifa duniani.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, NCSC  ina uhakika kwa kiwango cha juu kuwa GRU huenda ilihusika na mashambulizi kadhaa ya kimatandao ikiwa ni pamoja na yaliyofanywa dhidi ya chama cha Democratic nchini Marekani kabla ya uchaguzi mwaka 2016.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Jeremy Hunt amesema vitendo vya GRU havifai kwani vinajaribu kuhujumu demokrasia na kuingilia chaguzi katika nchi nyingine.

Hunt ameongeza kuwa ujumbe wao pamoja na washirika wao uko wazi na kuwa watafichua na kujibu jaribio lolote la GRU la kuhujumu uthabiti kimataifa.

Licha ya kutofahamika kama ilivyo kwa lililokuwa Shirika la Ujasusila uliokuwa Muungano wa Kisovieti (KGB), GRU ilihusika kwa kiwango kikubwa  katika baadhi ya matukio katika karne iliyopita ikiwa ni pamoja na wakati wa mgogoro wa makombora nchini Cuba na pia hatua ya kutwaliwa kwa jimbo la Crimea.

GRU ina mawakala duniani kote na inawajibika moja kwa moja kwa mkuu wa utumishi jeshini na pia kwa waziri wa ulinzi.

Mfumo wake wa kiutendaji, idadi ya wafanyakazi na masuala yake ya kifedha viko chini ya idara ya ujasusi ya Urusi.

Hata hivyo. GRU haizungumzii lolote juu ya vitendo vyake hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles