26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Kibaha Mjini akusanya milioni 4 ujenzi wa ofisi Serikali ya Mtaa

Na Gustafu Haule, Pwani

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvester Koka, amewaongoza wananchi katika harambee iliyokusanya Sh milioni 4.2 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mailimoja “A” uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha.

Katika harambee hiyo iliyofanyika jana, Koka amechangia kiasi cha Sh milioni tatu ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi na wadau wengine kujitokeza katika kuchangia ujenzi wa ofisi hiyo.

Mbunge huyo ameshirikiana na viongozi mbalimbali wa CCM na wananchi wa mtaa huo akiwemo Diwani wa Kata hiyo, Ramadhani Lutambi.

Jengo la ofisi hiyo linahitaji zaidi ya Sh milioni 12 mpaka kukamilika lakini katika harambee hiyo mbunge huyo alifanikiwa kukusanya Sh milioni 4.2 fedha ambazo zitasaidia katika hatua ya kwanza ya upauaji.

Pamoja na kupata fedha hizo, mbunge huyo ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau wengine katika kuhakikisha jengo hilo linakamilika huku akiagiza kuwafuatilia wananchi na wafanyabiashara waliopo karibu na eneo hilo.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha kwa harambee Koka amesema Serikali inadhamira kubwa ya kusogeza huduma karibu na jamii hasa kupitia ofisi za serikali ya mtaa.

Amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anafanyakazi kubwa ya kuijenga nchi na yeye anashuhudia jinsi anavyohangaika kutafuta fedha huku na kule.

Koka ameongeza kuwa utafutaji wa fedha unaofanywa na rais unalenga kujenga na kukamilisha miradi mikubwa nchi nzima lengo ni kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora kwa wakati.

“Rais wetu Mama Samia anafanyakazi kubwa na anadhamira ya dhati kwa Taifa la Tanzania ndio maana tumeona bajeti imefikia zaidi ya Trillioni 41 tofauti na awali ilivyokuwa chini ya Trillioni 40,”amesema Koka

Amesema rais anafanya mambo makubwa kiasi hicho ni vyema sasa wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, wabunge na kada nyingine wakajitoa katika kumsaidia Rais katika kutatua changamoto za wananchi katika Mitaa husika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mailimoja, Yassin Mudhihir amesema kuwa kwasasa wanafanyakazi katika nyumba ya kupanga jambo ambalo limekuwa ni gharama kubwa katika kuendesha ofisi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles