28.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

PURA kuwezesha zaidi Watanzania

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeahidi kuendelea kuimarisha ushiriki wa wazawa katika shughuli za petroli nchini ili kuhakkisha kuwa wanabobea katika nyanja hiyo.

Hayo yamebainishwa Julai 5, na Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Charles Sangweni wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo lilipo kwenye maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema malengo yao ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanabobea katika nyanja hiyo ya mafuta nchini kwa kupata elimu.

Amesema malengo yao ni kuhakikisha uzingatiaji wa vigezo vya kiafya,kiusalama na kimazingira katika shughuli za petroli ambapo wataimarisha ushiriki wa wazawa na manunuzi ya bidhaa na huduma za wazawa katika tasnia ya petroli.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli zinazofanyika katika uchakataji wa mafuta ghafi, kwenye kuchimba kwenye mkondo wa juu unapata mafuta ghafi au gesi lakini pia unaweza kuchimba visimana usipate kitu,” amesema Sangweni.

Amesema zaidi ya asilimia 60 ya gesi inatumika nchini katika maeneo mbalimbali ikiwamo kuzalisha umeme.

Amesema kuwa uchimbaji wa visima umekuwa na gharama kubwa ambapo kisima kimoja kinagharimu pesa milioni 80 ambapo jumla visima 96 vilichimbwa ni visima 44 pekee ndio vilipatikana na gesi na vingine 56 kukosa kabisa

“Kuwekeza kwenye sekta hii ni kujitolea sana Kwani unakua huna uwakika kama ukichimba utapata kitu hivyo serikali imeingia mikataba na wawekezaji Kwa kujua wao wakifanikiwa sehemu ya wanachokipata kinabaki nchini,”amesema.

Aidha amesema mamlaka hiyo humshaauri Waziri wa Nishati katika utoaji,usitishaji,ufutaji na uhuishaji wa leseni za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi.

Alieleza kuwa wanafanya kazi na serikali katika majadiliano ya mikataba ya ugawaji mapato PSA ambapo serikali huongea na wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali juu ya ugawaji wa vitalu na miradi ya kusindika gesi asilia kuwa kimiminika ikiwa ni pamoja na kutoa leseni ya usafirishaji wa gesi hiyo kwenye nje.

“Mamlaka hii tuna adhimia kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli kwa uwazi weledi na ufanisi ili kuchangia katika ustawi wa jamii na kiuchumi kwa watanzania na maslahi ya kizazi cha na kijacho,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles