31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu ashikiliwa na Polisi kwa mauaji ya mwanafunzi

Renatha Kipaka, Bukoba

Jeshi la polisi Mkoa wa Kagera linamshikiria mwalimu Adrian Tinchwa (36)kwa kosa la mauaji ya mwanafunzi Phares Buberwa (16) kidato cha tatu shule ya sekondari Igura iliyopo Kata ya Kanini Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amesema tukio hilo limetokea Septemba 18 majira ya saa 8 mchana eneo la Kakoni ambapo mtuhumiwa alimshambulia marehemu kwa kumpiga ngumi kwenye paji la uso na kutumia nondo kumpiga miguu na mikono hadi kusababisha majeraha makubwa.

Sababu ya shambulio hilo inadaiwa lilitokana na marehemu kutuhumiwa kuiba simu na kukata kufuli la nyumba na baada ya kutekeleza zoezi hilo alijaribu kukimbia ndipo mtuhumiwa huyo kukamatwa.

“Nisema tu ndungu waandishi Septemba 18, 2024 majira ya saa 3:00 asubuhi inasemekana mtuhumiwa aliingia nyumbani kwake na kukata kufuli la nyumba yake ambapo alipotaka kuingia ndani alikutana na marehemu mlango akiwa anatoka ndani,” amesema Kamanda Chatanda

Amesema mtuhumiwa alimpeleka marehemu nyumbani kwa wazazi wake akiwa amepata majeraha makubwa miwilini na kuwakabidhi ndipo wazazi hao walimkimbiza zahanati ya Rwambaizi ili apatiwe matibabu ya haraka ndipo alifariki.

Kamanda huyo amesema mtuhumiwa alishindwa kuzuia hasira yake na kutoa adhabu iliyopilitiza, uchunguzi unaendelea ili kupata ukweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles