22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

GBT yaja na fichua tukomeshe mashine haramu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika kuhakisha kuwa michezo ya kubahatisha inadhibitiwa hususan maeneo yenye makazi ya watu, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (GBT) imeanzisha kampeni ya Fichua, tukomeshe mashine haramu ambayo itahusisha wananchi.

Akizungumza na Mtanzania Digital katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea, Afisa Elimu na Uhusiano kwa Umma kutoka GBT, Zena Athuman amesema kampeni hiyo inahusisha wananchi kutoa taarifa wanapona mashine za michezo ya kubahatisha zinawekwa sehemu ambazo siyo rasmi.

“Lengo la kampeni hii ni kutaka wananchi kutoa taarifa wanapoona mashine hizi zinawekwa maeneo ambayo siyo kwama kwa mama ntilie, saluni, madukani na sehemu nyingine zenye makazi ya watu.

“Kwani maeneo yanayoruhusiwa kuwekwa mashine ni kwenye maduka maalum yanayotwa Slot na kwenye baa, hivyo kinyume na maeneo hayo basi mashine hiyo inakuwa haipo hapo kihalali maana haijarasimishwa kisheria,” amesema Zena.

Mashine zikiharibiwa.

Amesema kampeni hiyo ni ya ushirikishaji wananchi ili waweze kutoa taarifa mahala zilipo mashine hizo ili kwa kushirikiana na vyombo vya usalama ziweze kuteketezwa kote nchini.

“Tumekuwa na kampeni nyingi ambazo zimekuwa na matokeo mazuri sana, kwanxa tumebaini kwamba watu wanaoendesha mashine haramu ndiyo wamekuwa wakiruhusu watoto kucheza michezo hiyo jambo ambalo huwezi kulikuta kwa wamiliki halali waliofuata utaratibu.

“Mfano tulibaini watu wengi ambao wanendesha kinyume na utaratibu, Machi mwaka huu tumekamata na kuteketeza zaidi ya mashine 3,000 ambazo zilikuwa zikiendeshwa kinyume na utaratibu huku mikoa kama Arusha, Dar es Salaam na Mwanza ndiyo ilikuwa mikoa kinara,” amesema Zena.

Aidha, Zena ametoa wito kwa wananchi kutokushiriki katika mashine ambazo hajafuata utaratibu huku akihimiza jamii kutokutumia michezo hiyo kama sehemu ya kipato badala yake wafanye kama jambo la zaida la starehe.

“Tunahimiza wananchi kutokucheza michezo hii kwa matumaini badala yake wacheze kama burudani tena kutoka katika vipato vyao vya ziada,” amesema Zena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles