26.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 15, 2021

Mane awakaribia Salah, Gerrard

STAA wa Liverpool, Sadio Mane, jana alifunga moja katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Porto na hiyo ilimwezesha kuingia kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mane raia wa Senegal, sasa anakuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kufikisha mabao 20 katika historia ya michuano hiyo, akitanguliwa na Steven Gerrard (30) na Mohamed Salah (28).

Dhidi ya Porto, mchezo uliochezwa katika ardhi ya Ureno, nyota huyo alifunga bao la pili akitumia krosi ya ‘kiraka’ James Milner.

Haijasahaulika kuwa huu unakuwa msimu wake wa tano akiwa na Liverpool iliyomng’oa Southampton mwaka 2016.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,753FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles